Pata taarifa kuu
ULINZI-DIPLOMASIA

DRC: Wanajeshi wa Afrika Mashariki kuanza kujipanga upya Kivu Kaskazini

Jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) lilifafanua tarehe 9 Februari 2023 ramani yake mpya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). EAC inakusudia kujipanga upya katika mkoa wa Kivu Kaskazini, huku ikihakikisha usitishaji vita na M23 pamoja na kujiondoa Machi 2023 kwa uasi huu ambao unachukua maeneo kadhaa ya koa wa Kivu Kaskazini.

Wanajeshi wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishika doria huko Goma mnamo Desemba 2, 2022, siku tatu baada ya mashambulizi ya M23.
Wanajeshi wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishika doria huko Goma mnamo Desemba 2, 2022, siku tatu baada ya mashambulizi ya M23. AFP - GLODY MURHABAZI
Matangazo ya kibiashara

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mapigano yanaendelea kati ya jeshi na waasi wa M23. Mapigano hayo yamekaribia katika siku za hivi karibuni katika mji wa Sake huko Kivu Kaskazini, mji mkuu wa mwisho kabla ya Goma, mji mkuu wa mkoa huo.

Hali iliyopelekea Februari 4 kwenye kikao cha dharura cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Mkutano wa kilele ulifuatiwa Alhamisi, Februari 9 na mkutano wa wakuu wa majeshi wa ukand huo ambao walitayarisha ramani mpya ya kuonokana na mzozo huo.

Hati hii ya siri, ambayo ilivuja wikendi hii, ilithibitishwa na RFI. Kwa hivyo Wakuu wa Majeshi walirekodi kutoheshimiwa kwa makataa ya hapo awali yaliyoamuliwa katika mkutano wa kilele wa Wakuu wa Nchi ulioandaliwa mnamo Novemba 2022: usitishaji wa mapigano na uondoaji wa waasi wa M23 kutoka maeneo yaliyokaliwa.

Kuondioka kwa M23 kulibainishwa katika awamu tatu

Kwa sababu hiyo, Wakuu wa Majeshi wanapendekeza ramani mpya, kwa upande mmoja, kuanzishwa kwa utaratibu wenye jukumu la kuchunguza uheshimishwaji wa usitishaji mapigano. Wakati huo huo, bado kuna mazungumzo ya kujiondoa kwa M23.

Uondoaji ambao waraka unaeleza katika awamu tatu: kuanzia Februari 28 hadi Machi 10, unahusu Kibumba na Rumangabo, maeneo ambayo M23 pia wanatakiwa kuwa tayari wamerejea EAC, lakini pia maeneo yaliyotekwa hivi karibuni kwenye mhimili wa Sake-Butembo. Kuanzia Machi 13 hadi 20, lwatajiondoa kutoka maeneo ya kati ya Kivu Kaskazini, yale yanayozunguka mbuga ya Virunga na kuanzia Machi 23 hadi 30 kutoka ngome zilizotekwa mnamo mwezi Oktoba: Rutshuru na Kiwanja, lakini pia kutoka Bunagana, eneo la kwanza ambalo M23 ilichukua udhibiti mnamo mwezi Juni.

Mabadiliko mengine makubwa: kupelekwa tena kwa wanajeshi wa EAC katika Kivu Kaskazini. Wanajeshi wa Kenya hawatakuwa pekee tena wa kukalia maeneo yaliyokombolewa. Wanajeshi wa Burundi wataweka ngome zao kwa upande wa Masisi, Sudan Kusini watashirikiana na Wakenya kwenye mhimili wa kati ya Goma na Kaskazini mwa Rutshuru na Waganda wamekabidhiwa sehemu ya mashariki ya Rutshuru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.