Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Burkina, Mali na Guinea wakutana Ouagadougou

Wakuu wa diplomasia kutooka nchi tatu za Afrika Magharibi zinazoongozwa na jeshi kufuatia mapinduzi - Mali, Guinea na Burkina Faso - wamekutana Alhamisi huko Ouagadougou, serikali ya Burkina Faso imetangaza.

Mwanamke huyu akiwa ameshikilia bendera ya nchi yake na bendera ya Urusi huku watu wakikusanyika ili kuonyesha uungwaji mkono wao kwa kiongozi mpya wa kijeshi wa Burkina Faso Ibrahim Traore, mjini Ouagadougou, Januari 20, 2023.
Mwanamke huyu akiwa ameshikilia bendera ya nchi yake na bendera ya Urusi huku watu wakikusanyika ili kuonyesha uungwaji mkono wao kwa kiongozi mpya wa kijeshi wa Burkina Faso Ibrahim Traore, mjini Ouagadougou, Januari 20, 2023. REUTERS - VINCENT BADO
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unakuja siku mbili baada ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov nchini Mali siku ya Jumanne wiki hii, ambaye aliahidi msaada wake "kwa eneo la Sahel na hata kwa nchi zinazopakana na Ghuba ya Guinea".

Baada ya kikao chao cha kazi Abdoulaye Diop (Mali), Morissanda Kouyaté (Guinea) na Olivia Rouamba (Burkina Faso), wanatarajia kuwahutubia waandishi wa habari , kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Burkina Faso.

"Ni mara ya kwanza kwa mimi kufika Burkina Faso tangu mapambano ya wananchi wa Burkina Faso ambayo yalipelekea kuwepo na marekebisho ili kuweza kurejesha uhuru na uadilifu wa  nchi hii ndugu", ametangaza Abdoulaye Diop alipowasili nchini Burkina Faso.

"Kwa pamoja, tutatoa tamko kwa mashirika ya kikanda, ili tuweze kusikia hata kwa sauti zaidi malalamiko na maombi ya raia wetu kupitia serikali zetu na viongozi wetu", amesema kwa upande wake Morissanda Kouyaté.

Afrika Magharibi imekumbwa na msururu wa mapinduzi nchini Mali, Guinea na Burkina Faso tangu 2020, na kukosekana kwa utulivu kwa kanda ya Sahel inayokumbwa na ghasia za wanajihadi licha ya kutumwa kwa vikosi vya kimataifa na hivyo kutumwa kwa wanamgambo wa Urusi.

Baada ya Mali, Burkina Faso, ambayo pia imejaa umwagaji damu kutokana na ghasia za wanajihadi, imeomba tu kuondoka kwa vikosi vya Ufaransa kwenye ardhi yake, bila hata hivyo kuzingatia kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia na Ufaransa, ukoloni wa zamani katika eneo hilo.

Mamlaka zilizotokana na mapinduzi ya Septemba 30, 2022 yaliyofanywa na Kapteni Ibrahim Traoré, wa pili katika kipindi cha miezi minane, zimeelezea nia yao ya kubadilisha ushirikiano wao.

"Kwa kweli tunataka kuangalia mambo mengine, kwa sababu tunataka ushirikiano wa kushinda adui," Kapteni Traoré alisema wiki iliyopita, na kuongeza: "Ikiwa hatuwezi kumudu kununua zana za kijeshi katika nchi kama hii, tutakwenda nchi nyingine kuzitafuta".

Kulingana na nchi za Magharibi, mamluki kutoka kundi la Wagner wa Urusi wako nchini Mali, jambo ambalo Bamako inakanusha, ikitambua tu uwepo wa wakufunzi wa Urusi. Kapteni Traoré pia alikanusha kuwepo kwa mamluki wa Wagner nchini Burkina Faso, akisema kwamba "Wagner wetu ni VDP", 'watu waliojitolea kulinda uhuru wa taifa', wasaidizi wa kiraia wa jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.