Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Burkina: Wafanyakazi 2 wa MSF wauawa katika shambulio Kaskazini Magharibi

Timu ya shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) ilishambuliwa nchini Burkina Faso Jumatano Februari 8, shirika hilo likilaani mauaji ya wafanyakazi wake wawili, raia a Burkina Faso, na kusitisha shughuli zake za matibabu katika eneo la Boucle du Mouhoun, kaskazini-magharibi mwa nchi, ambako shambulio hilo lilitokea.

Shirika lisilo la kiserikali la Madaktari Wasio na Mipaka limelaani mauaji ya wafanyakazi wake wawili katika shambulio la Februari 8, 2023 nchini Burkina Faso.
Shirika lisilo la kiserikali la Madaktari Wasio na Mipaka limelaani mauaji ya wafanyakazi wake wawili katika shambulio la Februari 8, 2023 nchini Burkina Faso. © Lou Roméo / RFI
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika la MSF, timu ya wafanyakazi wake ililengwa kwa shambulio la risasi Jumatano asubuhi, kwenye barabara kati ya Dédougou na Tougan.

Gari walimokuwemo wafanyakazi wake hata hivyo, lilitambuliwa kwa uwazi kuwa mali ya MSF, ndai yake likiwa na wafanyakazi wanne.

Wafanyakazi wawili, raia wa Burkina Faso waliuawa katika shambulio hilo, mmoja ni dereva mwenye umri wa miaka 39 na mwingine alikuwa msimamizi wa vifaa, huku wenzaowawili wakinusurika shambulio hilo.

Mkuu wa MSF Dkt Isabelle Defourny amesema wamekasirishwa na kitendo hiki kiovo ambacho pia amekiita cha kikatili.

Ni shambulio la makusudi, itatubidi kujadili haraka na wahusika wote kwenye mzozo ili kuelewa kilichotokea. amesema Dk. Isabelle Defourny.

Boucle du Mouhoun ni eneo linalopatikana magharibi mwa Burkina Faso, kaskazini mwa Bobo-Dioulasso, eneo linalopakana na nchi ya Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.