Pata taarifa kuu
USALAMA-UGAIDI

Mapigano na wanajihadi nchini Mali: Idadi ya wanajeshi waliouawa yafikia 14

Wanajeshi 14 wa Mali waliuawa na kumi na mmoja kujeruhiwa siku ya Jumanne katika mapigano na wanajihadi katikati mwa nchi Januari 10, 2023, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa Alhamisi na jeshi la Mali, FAMA.

Gari la jeshi la Mali likiwa katika doria katikati mwa nchi, mnamo Februari 2020.
Gari la jeshi la Mali likiwa katika doria katikati mwa nchi, mnamo Februari 2020. AFP - MICHELE CATTANI
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya awali ilibaini siku moja kabla kuwa wanajeshi wasiopungua 12 wa Mali waliuawa wakati wa mapigano haya ambayo yalitokea kati ya miji ya Mopti na Ségou baada ya mashambulizi kadhaa dhidi ya jeshi kwa mabomu ya yaliyotengenezwa kienyeji. "Upande wa adui", jeshi la Mali linadai kuwa limeangamiza "magaidi 31", katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP.

Mali imekuwa inakabiliwa na mashambulizi ya wanajihadi tangu mwaka 2012 na mgogoro mkubwa katika nyanja nyingi, kisiasa, kiuchumi na kibinadamu. Katikati mwa nchi ni moja wapo ya maeneo yanayokumbwa na machafuko ambayo yameenea katika nchi jirani, Burkina Faso na Niger, na yamezikumba nchi za kusini mwa Mali.

Wanajeshi ambao waliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mnamo 2020 na kuimarishwa na mapinduzi ya pili mnamo 2021 wamejitenga na mshirika wa zamani,  Ufaransa, na washirika wake, na kushirikiana na Urusi kijeshi na kisiasa. utawala wa kijeshi ulizindua operesheni iliyolenga katikati mwa Mali mwishoni mwa mwaka 2021. Wananadai kuwatimua wanajihadi baada ya kuzindua mashambulizi makubwa kote nchini.

Katika ripoti ya katibu mkuu wa umoja wa Mataifa iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, umoja huo unaandika kinyume chake kwamba hali ya usalama iliendelea kuzorota kati ya mwezi Juni na Desemba 2022 katikati mwa Sahel, "hasa nchini Burkina Faso na Mali". "Nchini Mali, baada ya kuondoka kwa vikosi vya kimataifa, makundi yenye silaha yalisonga mbele mashariki mwa nchi, yakichukua udhibiti wa maeneo makubwa ya mpaka na Niger," ripoti hiyo inasema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.