Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Wanajeshi watatu wa Mali wauawa katika mapigano na wanajihadi

Wanajeshi watatu wa Mali waliuawa na watano kujeruhiwa siku ya Jumanne wakati wa mapigano na wanajihadi katikati mwa nchi, jeshi limesemakwenye mitandao ya kijamii.

Wanajeshi wa Jeshi la Mali (FAMA) wakishika doria huko Anderamboukane, katika jimbo la Menaka, 22 Machi 2019.
Wanajeshi wa Jeshi la Mali (FAMA) wakishika doria huko Anderamboukane, katika jimbo la Menaka, 22 Machi 2019. Agnes COUDURIER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jeshi linasema "limewaangamiza" wanajihadi saba wakati wa mapigano haya yaliyotokea kati ya maeneo ya Mopti na Ségou baada ya mashambulizi kadhaa kufanywa kulingana na jeshi hilo kwa kutumia vilipuzi dhidi ya wanajeshi wake.

Mali imekuwa inakabiliwa na mashambulizi ya wanajihadi tangu mwaka 2012 na mgogoro mkubwa katika nyanja nyingi, kisiasa, kiuchumi na kibinadamu. Katikati mwa nchi ni moja wapo ya maeneo yanayokumbwa na machafuko ambayo yameenea katika nchi jirani, Burkina Faso na Niger, na yamezikumba nchi za kusini mwa Mali.

Waajeshi ambao waliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mnamo 2020 na kuimarishwa na mapinduzi ya pili mnamo 2021 wamejitenga na mshirika wa zamani,  Ufaransa, na washirika wake, na kushirikiana na Urusi kijeshi na kisiasa. utawala wa kijeshi ulizindua operesheni iliyolenga katikati mwa Mali mwishoni mwa mwaka 2021. Wananadai kuwatimua wanajihadi baada ya kuzindua mashambulizi makubwa kote nchini.

Katika ripoti ya katibu mkuu wa umoja wa Mataifa iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, umoja huo unaandika kinyume chake kwamba hali ya usalama iliendelea kuzorota kati ya mwezi Juni na Desemba 2022 katikati mwa Sahel, "hasa nchini Burkina Faso na Mali". "Nchini Mali, baada ya kuondoka kwa vikosi vya kimataifa, makundi yenye silaha yalisonga mbele mashariki mwa nchi, yakichukua udhibiti wa maeneo makubwa ya mpaka na Niger," ripoti hiyo inasema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.