Pata taarifa kuu

Mjadala juu ya mustakabali wa Kifaransa nchini Mali, nchi yenye lugha 70

Mistari michache katika rasimu ya Katiba imefufua mjadala wa zamani nchini Mali: Kifaransa, lugha ya walowezi ambao sasa wameondoka, je, inapaswa kubaki kuwa lugha rasmi pekee ya nchi ambayo ina makumi ya lugha?

Swali liliibuka tena kwa kuwasilishwa mwezi Oktoba maandishi ambayo yanaweza kuwa Katiba mpya ya nchi.
Swali liliibuka tena kwa kuwasilishwa mwezi Oktoba maandishi ambayo yanaweza kuwa Katiba mpya ya nchi. Google Maps
Matangazo ya kibiashara

Fursa ya kupanua hadhi hii kwa baadhi ya nahau nyingi zinazotumiwa kila siku kuliko ile ya mkoloni wa zamani imeibuka tena tangu Mali, mkusanyiko mkubwa wa makundi ya watu, kupata uhuru mnamo 1960.

Swali liliibuka tena kwa kuwasilishwa mwezi Oktoba maandishi ambayo yanaweza kuwa Katiba mpya ya nchi.

Lugha zinachukua moja tu ya Ibara 195 za nakala hii iliyowasilishwa na utawala wa kijeshi madarakani kama moja ya mageuzi muhimu ya kuokoa nchi inayokabiliwa na kuenea kwa harakati za kijihadi na migogoro mingi. Lakini makala hii imefufua mjadala wa zamani kwenye runinga na kwenye "grin", kongamano lisilo rasmi ambapo raia wa Mali wanajadili kila kitu mezani.

"Je, ni kawaida kwamba, miaka 60 baada ya uhuru, Kifaransa ndiyo lugha yetu pekee rasmi?" anauliza Bamakois, Ali Guindo, mbele ya makazi yake katika wilaya ya Torokorobougou huko Bamako. "Tuna lugha nyingi hapa Mali, itakuwa vyema kuziweka katika utamaduni wetu rasmi".

Zaidi ya lugha 70 zinazungumzwa nchini Mali, 13 zimetambuliwa kama lugha za kitaifa, na moja tu, ya kigeni, Kifaransa, inatambuliwa rasmi, amekumbusha Amadou Salifou Guindo, mtaalamu wa isimu-jamii. Kifaransa hutumiwa katika utawala, kwenye ishara za barabarani, kwenye televisheni ya serikali, lakini kidogo sana mitaani huko Bamako, na hata vijijini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.