Pata taarifa kuu

Uingereza kuwaondoa wanajeshi wake katika kikosi cha MINUSMA

Uingereza imesema itawaondoa wanajeshi wake 300 kwenye jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa  MINUSMA nchini Mali, kufuatia hatua za nchi nyingine za Magharibi kuchukua hatua hiyo.

Askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha MINUSMA akishika doria karibu na Msikiti Mkuu wa Timbuktu, Desemba 9, 2021.
Askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha MINUSMA akishika doria karibu na Msikiti Mkuu wa Timbuktu, Desemba 9, 2021. © AFP - FLORENT VERGNES
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi James Heappey amewaambia wabunge kuwa, wanajesji wa Uingereza wanaondoka kwa sababu kuendelea kwa mapinduzi ya kijeshi nchini Mali, kunazuia jitihada za Jumuiya ya Kimataifa kuleta utulivu nchini humo. 

Hatua hii ya Uingereza imekuja baada ya Ufaransa kuamua kuwaondoa maelfu ya wanajeshi wake nchini Mali, kufuatia uongozi wa kijeshi katika taifa hilo la Afrika Magharibi, kuanza kushirikiana na kundi la kibinafsi la usalama la Wagner kutoka  nchini Urusi. 

Kuondoka kwa wanajeshi wan chi hizo za Ulaya, kunazua wasiwasi miongoni mwa wanadiplomasia kuwa hali ya usalama itaendelea kuwa mbaya katika nchi hiyo na nchi jirani na vita dhidi ya makundi ya kijihadi, vitayumba. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.