Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

DRC: Mashambulizi ya M23 yanaonekana kushika kasi Kivu Kaskazini

Jumamosi hii asubuhi, kulingana na vyanzo kadhaa, waasi wameteka maeneo ya kimkakati ya Rutshuru na Kiwanja, yapata kilomita 70 kaskazini mwa Goma. Kundi la waasi wa M23 waldai jana usiku, Ijumaa, waliteka kituo cha mpakani cha Kitagoma kwenye mpaka kati ya DRC na Uganda, takriban kilomita ishirini kaskazini mwa Bunagana.

Moja ya maeneo ya mji wa Rumangabo, Rutshuru, DRC, Oktoba 10, 2022.
Moja ya maeneo ya mji wa Rumangabo, Rutshuru, DRC, Oktoba 10, 2022. © Paulina Zidi / RFI
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji hao wa M23 walikuwa katikati ya Rutshuru saa nane mchana kwa saa za Mashariki mwa DRC.

Mmoja wa wasemaji wao, alifanya mkutano mfupi papo hapo kwa lugha ya Kiswahili, akitoa maelekezo na kuwataka wananchi wasiwe na hofu.

Huko Kiwanja, kuingia kwa wanajeshi wa M23 kulitanguliwa na milio ya silaha za kivita kuzunguka jiji hilo. Kama ilivyokuwa katikati ya Rutshuru, huko pia, hakukuwa na mapigano katika maeneo yanayokaliwa na watu.

Tangu alasiri, shughuli zilianza tena, ingawa wakazi wa mji huo walikuwa na woga.

Hata hivyo, kwa kuhofia usalama wao, baadhi ya waandishi wa habari, wanaharakati na wanachama wa mashirika ya kiraia walitafuta hifadhi katika kambi ya MONUSCO.

M23 ambayo inachukuliwa na Kinshasa kama kundi la kigaidi, bado linadai kufunguliwa kwa mazungumzo ya moja kwa moja na serikali. Hoja ambayo inafutiliwa mbali kabisa na Felix Tshisekedi ambaye anachagua njia ya kijeshi, akijiamini hasa juu ya kupelekwa kwa kikosi cha baadaye cha jumuiya ya Mataifa ya Afrika Mashariki.

Mkazi mmoja aliyehojiwa na Robert Minangoy wa Idhaa ya Kiswahili ya RFI,ameelezea masikitiko yake.

Tumekata tamaa... FARDC waliacha ngome zao na waasi wakaingia mjini... raia wanaishi mpaka sasa kwa huruma wa waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.