Pata taarifa kuu

Somalia: Idadi ya waliofariki katika shambulio mjini Mogadishu yaongezeka hadi 21

Nchini Somalia, idadi ya vifo inaongezeka baada ya mashambulizi ya wanamgambo wa Al-Shabaab dhidi ya hoteli moja katika mji mkuu, Mogadishu. Wizara ya Afya imetangaza Jumapili Agosti 21 kwamba watu wasiopungua 21 waliuawa na 117 kujeruhiwa katika shambulio la hoteli ya Hayat. Shambulio hilo lilimalizika Jumamosi jioni baada ya mapigano ya saa 30 kati ya Al Shabab na vikosi vya usalama vya Somalia.

Paa la hoteli ya Hayat mjini Mogadishu liliharibiwa kabisa kufuatia mapigano kati ya vikosi vya usalama na wanamgambo wa Al Shabab.
Paa la hoteli ya Hayat mjini Mogadishu liliharibiwa kabisa kufuatia mapigano kati ya vikosi vya usalama na wanamgambo wa Al Shabab. AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yalichukua muda wa saa thelathini. Hili halijawxahi kutokea Mogadishu, ingawa mji mkuu wa Somalia huwa mara kadhaa unakumbwa na mashambulizi ya Al Shabab.

"Naweza kuwaambia kwamba kilichotokea hapa ni maafa ambayo yamekuba famili nyingi katika ngazi zote, iwe ni idadi ya vifo au uharibifu wa mali. Kuzingirwa kwa hoteli hiyo kulichukua takriban saa 32. Vikosi vya usalama na wanamgambo wa Al Shabab walipigana mbele ya macho yetu. Kama unaweza kuona, kuna majengo mengi yaliyoharibiwa hapa. Matukio ya aina hii hujirudi mara kwa mara na sisi vijana ndio ambao huwa tunalengwa na mashambulizi hayo, " amesema mmoja wa mashuhuda

Viongozi wa Somalia wamejaribu kuhakikishia raia, wakiwatangazia kwamba wameokoa mateka 106, wengi wao wanawake na watoto.

Baada ya shambulio hili, maswali mengi yamebakia bila majibu: je, hoteli hii inayotembelewa na mawaziri na maafisa wa serikali inawezaje kulengwa? Kwa nini haikulindwa vyema zaidi?

Pia kuna masuala ya familia za watu waliopotea. Jumapili hii asubuhi, walikuwa wamekusanyika katika barabara inayoelekea hotelini, lakini waliwekwa kando na vikosi vya usalama, wakisubiri habari za ndugu zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.