Pata taarifa kuu
SOMALIA

Watu 13 wauawa nchini Somalia kufuatia shambulio la kigaidi mjini Mogadishu

Watu 13 wameuawa jijini Mogadishu nchini Somalia, kufuatia makabiliano ya saa kadhaa kati ya wanajihadi waliovamia hoteli ya kifahari na maafisa wa usalama.

Hoteli ya Hayat iliyoshambuliwa jijini Mogadishu, 19/08/2022
Hoteli ya Hayat iliyoshambuliwa jijini Mogadishu, 19/08/2022 Abdalle Ahmed Mumin via REUTERS - ABDALLE AHMED MUMIN
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia shambulio hilo, imeongezeka siku ya Jumamosi baada ya shambulio hilo kutekelezwa na magaidi ya Al Shabab hapo jana katika hoteli ya Hayat ambayo hutumiwa na maafisa wa serikali.

Mbali na mauaji ya raia, zaidi ya watu wengine 40 wamejeruhiwa na wanaendelea kupata matibabu jijini Mogadishu, kwa mujibu wa Daktari Mohamed Abdirahman Jama.

Maafisa wa usalama ambao wamekuwa wakipambana na magaidi hao wanasema watafanikiwa kumaliza operesheni dhidi ya magaidi hao katika kipindi kifupi kijacho.

Magaidi wa Al Shabab, wamekiri kutekeleza shambulio hilo la Kwanza tangu kuchaguliwa kwa rais mpya Hassan Sheikh Mohamud mwezi Mei.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.