Pata taarifa kuu
Mali - Minusma

UN: Yasikitika kwa utawala wa Mali kumfurusha msemaji wake

Kikosi cha umoja wa mataifa kinacholinda usalama nchini Mali, Minusma, kimeeleza kusitikishwa kwake na utawala wa kijeshi nchini humo kumfurusha msemaji wake, ila kimeahidi kuendelea kutekeleza majukumu yake nchini Mali.

Kikosi cha MINUSMA Julai 14, 2013
Kikosi cha MINUSMA Julai 14, 2013 Marie-Lan Nguyen / Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Serekali ya Mali imeagiza,  Olivier Salgado, kuondoka nchini humo kwa kipindi cha saa 72 zijazo, kutokana na taarifa yake aliyochapisha kwa mtandao wa twita kuhusiana na kukamatwa kwa wanajeshi wa Ivory Coast, taarifa ambayo utawala wa Mali umesema haikubaliki.

Bwana Salgado alikuwa amekanusha taarifa ya serikali ya Bamako kuwa haikujulishwa kuhusu ujio wa wanajeshi 49 wa Ivory Coast, ambao Bamako inawatumu kuwa mamluki waliolenga kuyumbisha serikali ya Mpito.

Mvutano kati ya serikali ya Mali na Minusma unatishia vita dhidi ya wanajihadi ambao wameendelea kutekeleza mashambulio.

Vuguvugu  linalounga mkono serikali, Yerewolo Debout sur les Remparts, linatarajiwa kuandaa mandamano terehe 29 mwezi huu, kushinikiza Minusma kuondoka nchini Mali kufikia Septemba 22 mwaka huu, siku  ambayo Mali huadimisha siku yake ya  uhuru wa Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.