Pata taarifa kuu
Mali - MINUSMA

Mali : Msemaji wa MINUSMA atimuliwa

Serikali ya kijeshi nchini Mali, imemtaka msemaji wa Jeshi la Umoja wa Mataifa MINUSMA kuondoka nchini humo, kufuatia maandishi katika ukurasa wake wa Twitter, yanayohusiana na kukamatwa kwa wanajeshi wa Ivory Coast nchini humo.

Cincina au Mali
Cincina au Mali © RFI
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Bamako kwenye taarifa yake  ,imesema msemaji huyo  Olivier Salgado, ana saa 72 kuondoka nchini Mali ,kufuatia habari alizochapisha kwenye mtandao wake wa Twitter , wakati huu kukiwa na mvutano kati ya utawala wa kijeshi wa Mali na washirika wa kimataifa ,wanaotuhumiwa kuwaunga mkono wanajihadi .

Mali  inakituhumu kikosi cha MINUSMA kwa kusalia kimya baada ya kutakiwa kutoa maelezo kuhusu habari alizochapisha Salgado.

Tangazo hilo linakuja pia siku chache baada ya mamlaka kuwamakata wanajeshi 49 wa Ivory Coast waliotajwa kuwa mamluki na serikali ya Bamako, na kwamba  walikuwa wamepanga njama ya kuipindua serikali ya kijeshi, madai ambayo Abidjan imekanusha na kutaka wanajeshi wake kuachiliwa huru mara moja na kusema walikwenda kufanya kazi za kikosi cha Umoja wa Mataifa.

 MINUSMA imekuwa ikifanya operesheni zake tangu mwaka 2013 kusaidia kupambana na wanaJihadi ambao wametekeleza mauaji nchini humo na katika nchi za eneo la Sahel na wengine kuyakimbia makawao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.