Pata taarifa kuu
Pembe ya Africa - baa la njaa

Njaa yasabisha vifo pembe ya Afrika

Mashirika ya kibanadamu yameonya kuwa raia katika mataifa ya Ethiopia, Kenya na Somalia, wanafariki kila baada ya sekunde 48 kutokana na baa la njaa, ambalo limesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, vita kati ya mataifa na kuongezeka kwa bei ya vyakula.

Lori la shirika la mpango wa chukula duniani
Lori la shirika la mpango wa chukula duniani Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya shirika la Oxfam na Save the Children, imekadiria kuwa zaidi ya watu millioni 181 kote duniani, wataathirika na baa la njaa mwaka huu, kwa mjibu wa ripoti hiyo ni kwamba wanawake wataathirika zaidi.

Ripoti ya mashirika hayo imeongeza kuwa hali hii inashuhudiwa kutokana na viongozi wa kisiasa kukosa kuweka mikakati ya kutosha kuzuia baa la njaa kuathiri raia.

Mashirika hayo pia yamelaumu jamii ya kimataifa kwa kutoa misaada kwa mataifa yalioathirika muda ukiwa umeyoyoma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.