Pata taarifa kuu
PEMBE YA AFRIKA-NJAA

Mataifa ya pembe ya Afrika yapo katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa

Ripoti mpya ya umoja wa Mataifa kuhusu njaa, imeonya kuhusu hali kuwa mbaya zaidi kwenye nchi za Pembe ya Afrika, Kuanzia Ethiopia, Kenya na Somalia, ambako kunashuhudiwa ukame kwenye baadhi ya maeneo, raia milioni 20 wakikabiliwa na baa la njaa.

Hali ya ukame katika nchi za pembe ya Afrika
Hali ya ukame katika nchi za pembe ya Afrika AP - Michael Tewelde
Matangazo ya kibiashara

Umoja huo umesema watu ambao wameathirika ni jamii zinazotegemea mifugo na kilimo cha kujikimu ,na kwa misimu minne mfululizo ,hawajapokea mvua tangu mwaka 2020 na hali hii ikifanywa kuwa mbaya zaidi na uvamizi wa nzige waliofagia mashamba yao.

Shirika la mpango wa chakula duniani ,WFP,imesema idade hiyo inaweza ikaongezeka,taifa la Somalia,likichangia watu milioni sita,Ethiopia ,milioni sita nukta tano na wakenya wakiwa ni watu milioni tatu nukta tano.

Shirika la umomja wa mataifa ,linalowashughulikia watoto ,UNICEF,limesema karibu watoto milioni mbili kwenye ukanda huo,wameathirika na utapiamlo, na ukosefu wa maji safi ulikuwa unawaweka watoto wengi kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa na wengi kuacha shule.

Kando na athari hiyo ya ukame kwa binadaam,umoja wa mataifa aidha umeonya kuhusu kuongezeka mizozo ya binadaam na wanyama pori.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.