Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Burkina Faso: Watu saba wauawa katika shambulizi Arbinda

Watu saba waliuawa Jumatatu asubuhi katika shambulio la kigaidi huko Arbinda, eneo la Sahel kaskazini mwa Burkina Faso. Wahanga hao wanne ni watu wa kujitolea kwa ajili ya ulinzi wa nchi, wengine watatu ni raia, akiwemo mwanamke.

Eneo la Arbinda, Burkina Faso.
Eneo la Arbinda, Burkina Faso. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Tukio hili linakuja siku moja baada ya mashambulizi mawili yaliyoua watu 15 siku ya Jumatatu karibu na mji wa Dori, takriban kilomita mia moja mashariki mwa Arbinda.

Ilikuwa kwenye kituo cha kusambaza maji, kusini-magharibi mwa viunga vya Arbinda ambapo watu wenye silaha walishambulia Jumatatu, Machi 15 asubuhi. Kulingana na Ouarem Boureima, meya wa zamani wa jiji hilo, harakazi zao kutekeleza ukatili zinasalia jinsi zilivyo: watu kumi na wawili waliwasili kwa pikipiki, na kuanza kuharibu visima vay maji, pampu na kushambulia raia na baadae kuondoka.

“Ni unyanyasaji wa kweli, amesemammoja wa wabunge. Kwa muda wa wiki tatu wamekuwa wakiharibu vyanzo vyetu vya maji ya kunywa na kujaribu kutukosesha amani”. Leo, karibu nusu ya vituo vya maji vya jiji vimeharibiwa. Barabara zinazotumiwa kwa usafiri pia zinalengwa. Siku ya Jumatatu, basi lililokuwa likielekea mji wa Dori lilikanyaga mobu la kutegwa ardhini na kuua watu wawili. Wanajeshi waliotumwa kuingilia kati walishambuliwa na 13 kati yao waliuawa.

Magaidi wanataka kuteka eneo hilo

Kwa wiki kadhaa, magaidi wamekuwa wakitekeleza mkakati wa hifadhi kwa eneo hili, kinaeleza chanzo cha usalama cha Ufaransa. "Wanataka kuwafukuza wakazi wa eneo hilo ili waweze kupiga kambi huko na kupanga aina ya vizuizi kwa hili. »

Mwanzoni mwa mwaka huu, Operesheni Barkhane na vikosi vya jeshi vya Burkina Faso vilishirikiana katika hatua kadhaa dhidi ya kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Ansarul Islam katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.