Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-SIASA

Burkina Faso: Tume yapendekeza muda wa miezi thelathini kabla ya uchaguzi

Nchini Burkina Faso, tume iliyoundwa mapema Februari kufanyia kazi rasimu ya katiba ya mpito, iliwasilisha ripoti yake kwa rais Jumatano hii, Februari 23, 2022, baada ya wiki mbili za kazi. Imependekeza kipindi cha mpito cha miezi thelathini kabla ya kuandaa uchaguzi.

Mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.
Mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa tume hii, hasa raia, wakiwemo wanasheria, wanasosholojia, wanauchumi, na pia maafisa, walikabidhi hati zao kwa Paul Henri Sandaogo Damiba, ambaye alichukua madaraka mnamo Januari 24. Nakala hizo zimetaja kipindi cha mpito cha miaka miwili na nusu, kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na ofisi ya rais, ikiwa ni pamoja na chanzo cha kijeshi kilichonukuliwa na shirika la habari la AFP.

Serikali ya watu ishirini

Kwa mujibu wa vyanzo hivi, waraka ambao bado haujawekwa wazi, unatoa nafasi ya serikali ya watu wapatao ishirini na chombo cha kutunga sheria, chenye wajumbe wapatao hamsini. Inatarajiwa sasa kuwasilishwa kwa wadau mbalimbali kabla ya kuidhinishwa, kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na ofisi ya rais, ambacho kinabainisha kuwa tume hiyo ilitaka "kuzingatia matarajio ya jumuiya ya kimataifa".

Ripoti hii ina rasimu ya katiba ya mpito, ajenda ya mpito na mkataba wa kimaadili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.