Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA

Jitihada za kidiplomasia zaendelea kwa minajili ya kusitisha mapigano Tigray

Nchini Ethiopia, ziara rasmi zimeongezeka tangu wiki iliyopita na ujumbe wa usuluhishi wa Umoja wa Afrika unaoongozwa na Olusegun Obasanjo unaendelea kati ya serikali na waasi wa TPLF. Licha ya kuendelea kwa mapigano katika eneo la Afar, ishara nyingi zinaonyesha uwezekano wa hivi karibuni kuelekea usitishaji mapigano huko Tigray.

Kambi ya Emba Dansu, iliyopewa jina la shule ya msingi katika mji wa Shire ambapo wakazi wa Tigray Magharibi wamekimbilia, katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia, Mei 2021.
Kambi ya Emba Dansu, iliyopewa jina la shule ya msingi katika mji wa Shire ambapo wakazi wa Tigray Magharibi wamekimbilia, katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia, Mei 2021. © RFI/Sébastien Németh
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe maalum mpya wa Rais wa Marekani Joe Biden ndiye mtu muhimu zaidi aliyetua Addis Ababa katika siku za hivi karibuni. David Satterfield aliwasili Jumapili Februari 13 kwa ziara ya saa 48 ambapo alikutana na serikali, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu. Na aliwasili baada ya mjumbe maalum wa Umoja wa Ulaya katika Pembe ya Afrika, Annette Weber, na kisha naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohammed.

Wote walikuja na lengo la kupata makubaliano kati ya pande hasimu.

Amina Mohammed alikaribisha kwamba sasa kuna "uhasama mdogo kuliko miezi michache iliyopita" na kusema Ethiopia iko "katika nafasi nzuri zaidi" ya kutatua mzozo huo. Kuhusu Annette Weber, alibaini kwamba mazungumzo yalikuwa yakiendelea ili TPLF isichukuliwi tena kama "chombo cha kigaidi", na kwamba pia kulikuwa na mazungumzo kuhusu "usitishwaji wa mapigano" katika siku zijazo.

Wakati huo hio msaada a dharura kutoka shirika la Afya Duniani, WHO, hatimaye umeanza kupelekwa huko Mekele, mji mkuu wa jimbo la Tigray, tangu siku ya Ijumaa Februari 11: tani 33 za vifaa vya matibabu witapewa wahudumu wa afya ambao hawajapewa chochote, kwa wiki kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.