Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Maandamano yarindima Afar kati ya waasi na jeshi

Mapigano yameendelea kushuhudiwa kati ya waasi wa Tigray na wanajeshi wa serikali ya Ethiopia katika jimbo la Afar, karibu na mpaka wa Djibouti, licha ya jitihada za kidiplomasia kusitisha mapigano yanayoendelea katika taifa hilo la pembe ya Afrika. 

Mapigano haya yanaendLEea kusababisha maelfu ya watu kuyakimbia makwao katika jimbo hilo, wanaokadiriwa kuwa zaidi ya Laki tatu.
Mapigano haya yanaendLEea kusababisha maelfu ya watu kuyakimbia makwao katika jimbo hilo, wanaokadiriwa kuwa zaidi ya Laki tatu. AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

Licha ya jitihada hizo za kidiplomasia, kwa wiki mbili sasa, eneo la Kaskazini mwa Ethiopia, limeendelea kuwa uwanja wa vita, baada ya waasi wa Tigray kuvamia jimbo la Afar. 

Kuendelea kwa mapigano haya, kunaendelea kuzua maswali iwapo kweli, waasi wa Tigray wana nia ya dhati ya kusitisha vita na iwapo wana mipango ya kwenda jijini Addis Ababa au Djibouti. 

Mapigano haya yanaendelea kusababisha maelfu ya watu kuyakimbia makwao katika jimbo hilo, wanaokadiriwa kuwa zaidi ya Laki tatu. 

Aidha, mapigano hayo yanakwamisha misaada ya kibiandamu kama chakula na dawa kuwafikia watu wenye uhitaji katika jimbo la Tigray. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.