Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

DRC: Kundi la waasi la M23 laanzisha tena shughuli zake za kijeshi Kivu Kaskazini

Shambulio jipya lililohusishwa na "kundi la waasi la M23", ambalo pia linajiita Jeshi la Mapinduzi ya Kongo, siku ya Jumanne lililenga ngome za jeshi la DRC katika eneo la Rutshuru, kilomita kadhaa kaskazini mwa mji wa Goma.

Mwanajeshi wa DRC kwenye uwanja wa vita dhidi ya M23 huko Bunagana (picha ya zamani).
Mwanajeshi wa DRC kwenye uwanja wa vita dhidi ya M23 huko Bunagana (picha ya zamani). REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo inaonyesha takriban wanajeshi ishirini waliuawa wakati wa mapigano hayo, kulingana na vyanzo kutoka katika mkoa huo na mashirika ya kiraia.

Wanajeshi wa DRC wamethibitisha mapigano hayo lakini wamebaini kwamba hayakusababisha hasara kubwa. Hata hivyo wanathibitisha kuwa afisa wa jeshi ni miongoni mwa wanajeshi waliouawa.Shambulio hilo lililenga ngome ya jeshi karibu na Hifadhi ya Wanyama ya Virunga huko Nyesisi.

Kundi la waasi pia linaripotiwa kupata hasara katika mapigano hayo, lakini hakuna chanzo kutoka jeshi chanzo cha kiraia kinachothibitisha idadi ya waasi waliouawa au kujeruhiwa katika makabiliano hayo.

Gavana wa mkoa wa Kivu Kaskazini alizuru eneo la mapigano siku ya Jumatano kwa ziara ya "kuwafariji wanajeshi".

Mapigano yalikuwa bado yakiendelea jana. Jenerali Constant Ndima alisimamia operesheni yakurusha makombora dhidi ya maeneo ya waasi waliokuwa wakidhibiti milima ya Nyesisi na Ngugo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.