Pata taarifa kuu
DRC-HAKI

DRC: Watu kadhaa wakamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya balozi wa Italia Goma

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), polisi katika mkoa wa Kivu Kaskazini wanatangaza kwamba wamewakamata washukiwa wa shambulio ambalo balozi wa Italia Luca Attanasio, mlinzi wake na dereva wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, waliuawa Februari 22, 2021, karibu na mbuga ya wanyama ya Virunga.

Balozi wa Italia nchini DRC, Luca Attanasio, aliuawa na watekaji nyara mnamo Februari 22, 2021 karibu na Hifadhi ya Wanyama ya Virunga, mashariki mwa DRC.
Balozi wa Italia nchini DRC, Luca Attanasio, aliuawa na watekaji nyara mnamo Februari 22, 2021 karibu na Hifadhi ya Wanyama ya Virunga, mashariki mwa DRC. © Handout/AFP
Matangazo ya kibiashara

Majambazi hao, wakiwemo wanaodaiwa kuwa wahusika wa mashambulizi dhidi ya misafara ya magari ya mashirika ya kutoa misaada katika eneo hilo, walioneshwa Jumanne, Januari 18, kwa mamlaka ya kisiasa na kijeshi ya mkoa wa Kivu Kaskazini.

Watu hao sita, ambao bado ni vijana, walilazimishwa kukaa chini, huku wakizingirwa na maafisa wa polisi waliojihami kwa silaha za kivita. Walioneshwa kwa gavana wa mkoa wa Kivu Kaskazini na Jenerali Aba Van Ang, mkuu wa polisi: “Mmoja wa washukiwa hao alijinasibu kwa jina la Aspirant, yuko mafichoni. Walifanikiwa kutueleza kuwa walipomteka balozi wa Italia, mtu huyo ndiye aliyempiga risasi balozi. Walijuta sana kupoteza dola milioni moja kama fidia ambayo wangelipewa]. Kifo cha balozi kiliwafanya wapoteze pesa hizo.”

Utekaji nyara umeenda vibaya

Kwa hivyo ini operesheni ya utekaji nyara ambayo ilienda vibaya. Polisi wanatarajia, kutokana na taarifa walizopata, kumkamata mshukiwa huyo aliyempiga risasi balozi, ambaye kwa sasa yuko mafichoni. Katika eneo hilo, watekaji nyara hawa wanafanya kazi katika genge lililopangwa, polisi inasema.Waendesha pikipiki za kukodiwa wananyooshewa kidole na polisi kwa kuwasaidia wahalifu hao.

Kesi ili kuzuia uhalifu

Baadhi yao wamekiri kushiriki katika utekaji nyara wa wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada. Gavana wa mkoa wa Kivu Kaskazini anataka haki itendeke: “Haki itendeke. Waadhibiwe kwa maovu yote waliotendea raia”. Kesi imeanza. Mamlaka ya kisiasa na kijeshi inataka wahalifu kuhukumiwa katika kesi za umma ili kuzuia uhalifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.