Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Côte d'Ivoire: Alassane Ouattara na Henri Konan Bédié wasitisha mvutano kati yao

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara amekutana kwa mazungumzo na kiongozi wa muungano wa upinzani, Henri Konan Bédié. Mkutano huu ulifanyika siku mbili baada ya hotuba ya televisheni ya Alassane Ouattara ambapo alionyesha nia yake ya kukutana na kiongozi wa PDCI.

Alassane Ouattara na Henri Konan Bédié baada ya mkutano wao, Novemba 11, 2020.
Alassane Ouattara na Henri Konan Bédié baada ya mkutano wao, Novemba 11, 2020. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya kukamatwa kwa mwanasiasa mwingine wa upinzani Pascal Affi N’Guessan, hali ambayo imezua vurugu nchini humo na kusababisha vifo vya watu watatu.

Jean-Yves Le Drian, Waziri Mambo ya nje wa Ufaransa , amekuwa akithathmini jitihada za kuwepo kwa mazungumzo nchini humo.

Upinzani ulikuwa ukiandamana dhidi ya alassane Ouattara kuwania kwa muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais ambao alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo.

"Tumekubaliana kuwa amani ni jambo muhimu zaidi kwetu sote, na kwa wananchi wote wa Côte d'Ivoire," ametangaza rais wa alassane Ouattara, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi kuhusu kilichoafikiwa kwenye maungumzo hayo

Rais Ouattara amesema kwanza ilikuwa swala la "kurejesha imani" na kwamba "mazungumzo tayari yameanza vizuri", amesema mwandishi wetu huko Abidjan, François Hume-Ferkatadji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.