Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa urais Côte d’Ivoire: ECOWAS yatoa wito kwa utulivu

Ujumbe wa mawaziri wa ECOWAS ulitamatisha ziara yao ya siku mbili nchini Cote d'Ivoire, jana Jumatatu, wakati huu nchi hiyo ikijiandaa kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwezi huu.

Waandamanaji wanatawanyika na kukimbia baada ya maandamano katika wilaya ya Cocody dhidi ya muhula wa tatu wa Alassane Ouattara huko Abidjan mnamo Oktoba 19, 2020.
Waandamanaji wanatawanyika na kukimbia baada ya maandamano katika wilaya ya Cocody dhidi ya muhula wa tatu wa Alassane Ouattara huko Abidjan mnamo Oktoba 19, 2020. PATRICK FORT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi umewataka wanasiasa wa upinzani, Pascal Affi N'guessan wa FPI na Henri Konan Bedié wa PDCI kutafakari tena zaidi juu ya mpango wao wa kususia mchakato wa uchaguzi, huku wakitoa wito kwa raia kuasi.

Ujumbe huu unatolewa wakati huu kukiripotiwa mvutano mkubwa nchini humo. Kwa siku kadhaa, makabiliano makali yameanza tena, hasa katikati-mashariki mwa nchi lakini pia katika maeneo kadhaa ya mji wa Abidjan.

Angalau mtu mmoja aliripotiwa kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa Jumatatu wiki hii Kusini-Mashariki mwa Cote d'Ivoire wakati wa maandamano mapya dhidi ya rais Alassane Ouattara, ambaye anawania muhula wa tatu katika uchaguzi unaopangwa kufanyika Oktoba 31.

Vurugu hizo zilitokea katika mji wa Bonoua, karibu kilomita hamsini kutoka mji wa Abidjan, wakati vikosi vya usalama vilipowafyatulia risasi waandamanaji, mashahidi kadhaa wamebaini.

Picha zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha waandamanaji wakiwa wamembeba mtu kwenye machela ya chuma.

"Nilimwona kijana aliyeuawa. Wametembea katika eneo hili na mwili wake," amesema Pélagie Vangah, mmoja wa wafanyakazi katika eneo la Bonoua.

Afisa mmoja, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kwa upande wake kwamba aliona askari wa polisi wakimpiga risasi mwandamanaji anayepinga serikali. Waandamanaji wengine kadhaa wamejeruhiwa, aliongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.