Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Joto la kisiasa lapanda Cote d'Ivoire, wawili wajiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais

Wagombea wawili wa upinzani nchini Cote d'Ivoire wamejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania urais, wakati wa uchaguzi wa urais mwishoni mwa mwezi huu.

Pascal Affi N'Guessan, Agosti 27, 2020 huko Abidjan.
Pascal Affi N'Guessan, Agosti 27, 2020 huko Abidjan. AP Photo/Diomande Ble Blonde
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao Henri Konan Bédié na Pascal Affi N'Guessan, wametoa tangazo hilo baada ya kuanza kwa kampeni za kutafuta uongozi wa nchi hiyo katika uchaguzi ambao rais Ouattara anawania kwa muhula wa tatu.

Hayo yanajiri wakati upinzani nchini Côte d'Ivoire umetoa wito kwa wapiga kura na wanaharakati "kususia kikamilifu" kampeni za uchaguzi kwa "njia zote za kisheria"

Upinzani pia umetoa wito wa "kuzuia shughuli yoyote inayohusiana na uchaguzi" katika taarifa iliyosomwa na mgombea wa chama cha FPI, Pascal Affi N'Guessan, na la Henri Konan Bédié, mgombea mwingine wa chama PDCI aliyeidhinishwa na Mahakama ya Katiba.

Kwa mwezi mmoja mfululizo, upinzani umeendelea kutoa madai yanayoeleweka kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wowote. Madai hayo ni pamoja na kuondolewa Alassane Ouattara kwenye orodha ya wagombea. Hatua ya Alassane Ouattara kuwania katika uchaguzi huo kwa muhula wa tatu ni kinyume na Katiba ya nchi, kulingana na upinzani.

Upinzani unalaani "mapinduzi ya uchaguzi" yanayoandaliwa, na unataka kufunguliwa kwa mazungumzo kuhusu madai haya na kambi zote katika siasa nchini Côte d'Ivoire.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.