Pata taarifa kuu
MALI-SIASA-USALAMA

Mali: Rais wa Mali Keïta aendelea kushinikizwa kujiuzulu

Maelfu ya waandamanaji wa upinzani wamerejelea tena maandamano nchini Mali, kushinikiza kujiuzulu kwa rais Ibrahim Boubacar Keita na wWaziri wake mkuu Boubou Cissé.

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta, akiambatana na rais wa Niger Mahamadou Issoufou huko Bamako.
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta, akiambatana na rais wa Niger Mahamadou Issoufou huko Bamako. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Upinzani unamshtumu rais huyo kushindwa kupambana na ufisadi na utovu wa usalama.

Maneneo yaliyoandikwa kwenye mabango yanayobebelewa na waandamanaji yanamlenga rais Keïta, ambaye yuko madarakani tangu 2013, lakini pia Waziri wake Mkuu Boubou Cissé.

Haya ni maandamano ya kwanza dhidi ya utawala tangu upinzani kusitishwa maandamano yake Julai 21 kufuatia sikukuu ya Waislamu ya Eid al-Adha.

Mapema wiki hii majaji wapya katika Mahakama ya katiba waliapishwa nchini Mali, ikiwa ni mojawapo ya hatua ya kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa ambao umekuwa ukiendelea nchini humo kwa miezi kadhaa sasa.

Wito wa kumtaka rais huyo ajiuzulu umeongezeka baada ya maandamano ya hivi karibuni kujibiwa vikali na vikosi vya usalama, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 12.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.