Pata taarifa kuu
MALI-AMNESTY INTERNATIONAL-USALAMA

Vikosi vya usalama vya Mali vyahusishwa katika visa vya mauaji dhidi ya waandamanaji Mali

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limevishutumu vikosi vya usalama nchini Mali kwa kuhusika katika ukandamizaji na umwagaji damu" uliowalenga waandamanaji mwezi uliopita wakitaka kujiuzulu kwa Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta.

Waandamanaji wakibebelea mabango yaliyoandikwa "4IBK achia ngazi" wakati wa maandamano dhidi ya serikali.
Waandamanaji wakibebelea mabango yaliyoandikwa "4IBK achia ngazi" wakati wa maandamano dhidi ya serikali. MICHELE CATTANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Amnesty International inasema vikosi vya usalama viliuwa watu kadhaa kwa kuwapiga risasi na hii ni kulingana na mashuhuda kama alivyoeleza Ousmane Diallo mtafiti wa shirika hilo.

Rais Ibrahim Boubakar Keita ambaye amesalia na miaka mitatu tu katika muhula wake wa mwisho, anakabiliwa na shinikizo za kutaka ajiuzulu tangu mwanzoni mwa mwezi Juni.

Umaarufu wake umeshuka kutokana na madai ya ufisadi yanayoizonga serikali yake huku mzozo wa wapiganaji wa Kiislamu wenye itikadi kali ukiendelea kuitia doa serikali yake.

Wito wa kumtaka rais huyo ajiuzulu umeongezeka baada ya maandamano ya hivi karibuni kujibiwa vikali na vikosi vya usalama, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 12.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.