Pata taarifa kuu
NIGER-UFARANSA-USALAMA

Shambulio la Kouré nchini Niger: Emmanuel Macron aitisha kikao cha Baraza la Ulinzi

Baada ya shambulio ambalo liligharimu maisha ya wafanyakazi sita wa shirika la misaada ya kibinadamu kutoka Ufaransa na wenzi wao wawili kutoka Niger, rais wa Ufaransa ameitisha kikao cha baraza la ulinzi kutathmini hali mbambo kuhusu shambulio hilo.

Emmanuel Macron anaongoza kikao cha baraza la ulinzi asubuhi ya Jumanne hii baada ya shambulio huko Niger.
Emmanuel Macron anaongoza kikao cha baraza la ulinzi asubuhi ya Jumanne hii baada ya shambulio huko Niger. Christophe SIMON / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Emmanuel Macron ataongoza kikao hicho cha Baraza la Ulinzi kwa njia ya video. Atawakusanya pamoja Waziri Mkuu Jean Castex, Mawaziri wa Mambo ya nje, Ulinzi na Mambo ya ndani, na pia wakurugenzi na waratibu wanaohusika, hasa idara ya ujasusi.

Wakati huo huo jeshi la Niger, likisaidiwa na lile la Ufaransa wameanzisha msako wa kuwatafuta watu waliotekeleza mauaji ya watu wanane wakiwemo watalii sita kutoka nchini Ufaransa.

Nao wachunguzi nchini Ufaransa wameanzisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo yaliyotokea Jumapili iliyopita katika mji wa Koure, huku serikali ya Niger na Ufaransa wakiapa kuwapata waliohusika na mauaji hayo.

Mapema Jumatatu hii Paris ilithibitisha kwamba Wafaransa hao waliuawa katika shambulio hilo lililotokea Jumapili. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia alizungumza kwa simu na mwenzake wa Niger, Mahamadou Issoufou, Ikulu ya Elysee alisema.

Rais wa Ufaransa na mwenzake wa Niger waliapa kuendelea na vita dhidi ya makundi ya kigaidi huko Sahel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.