Pata taarifa kuu
NIGER-UFARANSA-USALAMA

Niger: Wafaransa sita na raia wawili wa Niger wauawa na watu wenye silaha katika eneo la Kouré

Watu wanane - Wafaransa sita na raia wawili wa Niger - wameuawa hivi punde na watu wenye silaha ambao walikuja kwa pikipiki katika eneo la Kouré, Kusini Magharibi mwa nchi, linalojulikana kama hifadhi ya mwisho ya Twiga huko Afrika Magharibi.

Picha hii iliyotolewa na AFP Agosti 9, 2020 inaonyesha gari walikuemo Wafaransa sita, na mkalimani wao mmoja na dereva, wote raia wa Niger waliouawa na watu wenye silaha, katika eneo la Kouré, Agosti 9, 2020.
Picha hii iliyotolewa na AFP Agosti 9, 2020 inaonyesha gari walikuemo Wafaransa sita, na mkalimani wao mmoja na dereva, wote raia wa Niger waliouawa na watu wenye silaha, katika eneo la Kouré, Agosti 9, 2020. AFP
Matangazo ya kibiashara

Paris imethibitisha kwamba Wafaransa wameuawa katika shambulio hilo lililotokea jana Jumapili, bila kutoa idadi ya wahanga. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia amezungumza kwa simu na mwenzake wa Niger, Mahamadou Issoufou, Ikulu ya Elysee amesema.

Jumapili hii, Agosti 9, katika mkoa wa Kouré, mashariki mwa mji mkuu wa Niger, watu wenye silaha waliwapiga risasi watu 8, ikiwa ni pamoja na raia wawili kutoka Niger na Wafaransa sita.

Habari hiyo ilitolewa na shirika la Habari la AFP na kuthibitishwa kwa RFI na Tidjani Ibrahim Katiella, Gavana wa mkoa wa Tillabéri.

Watu wanane waliuawa, Wafaransa sita na raia wawili kutoka Niger. Majambazi wenye silaha waliokuwa katika magari ndio walihusika na vifo vya raia hao katika eneo la kitalii la Kouré. Eneo hili ni hifadhi ya Twiga, Twiga wa mwisho katika Afrika Magharibi. Tumeanzisha uchunguzi na tumeanza pia kuwasaka majambazi hao katika eneo hilo. Tuna huzuni mkubwa, na ni tukio la kusikitisha kwa kweli. Ktika siku za hivi karibuni, tulikuwa katika hali ya utulivu, tumeshtushwa na tukio hilo, inauma kwa kweli, amesema Gavana wa mkoa wa Tillabéri akihojiwa na Charlotte cosset.

Rais wa Ufaransa na mwenzake wa Niger wamebaini kwamba watafanya kilio chini ya uwezo wao ili kubaini mazingira ya mauaji hayo katika saa za hivi karibuni. Wameapa kuendelea na vita dhidi ya makundi ya kigaidi huko Sahel.

Baraza la ulinzi litakutana Jumanne asubuhi chini ya uenyekiti wa rais wa Ufaransa kulingana na taarifa zitakuwa zimetolewa leo Jumatatu Agosti 10 na viongozi wa Niger na Ufaransa. Wizara ya mambo ya ndani ya Niger limesema kuwa operesheni ya kusaka majambazi hao inaendelea, ambapo jeshi la Barkhane linashiriki.

Rais wa Niger Mahamadou Issoufou, ambaye alizungumzia kuhusu "shambulio la kigaidi na kikatili", ameongea kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kwa kutoa rambirambi zake kwa familia za wahanga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.