Coronavirus: Afrika Kusini yajitaarisha kulegeza vizuizi zaidi
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema analenga kulegeza masharti zaidi ya watu kuendelea na shughuli zao za kawaida, wakati huu nchi hiyo inapoendelea kukabiliana na janga la Corona.
Imechapishwa:
Hata hivyo, amesema maeneo ambayo kuna maambukizi zaidi, shughuli za kawaida zitaanza kurejea polepole mwezi Juni, huku akisisitiza kuwa lengo ni kuanza kurejesha nchi hiyo katika mfumo wake wa kawaida wa kiuchumi.
Afrika Kusini ina visa vya Corona zaidi ya Elfu 12, watu 4,745 wamepona na 219 wamefariki dunia kutokana na virusi hivyo.
Takribani watu 300,000 kote duniani wameripotiwa kufariki dunia kutokana na virusi vya Corona, na zaidi ya visa milioni 4.3 vimerekodiwa.