Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-CORONA-UCHUMI

Maambukizi ya virusi vya Corona yapindukia 5,350 Afrika Kusini

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Afrika Kusini imefika watu 5,350 baada ya visa vipya 354 kuthibitishwa, huku idadi vifo ikifikia watu 103, imesema wizara ya afya.

Afisa wa afya wakati wa kampeni ya kufanya vipimo vya virusi vya Corona huko Lenasia, Afrika Kusini Aprili 21, 2020.
Afisa wa afya wakati wa kampeni ya kufanya vipimo vya virusi vya Corona huko Lenasia, Afrika Kusini Aprili 21, 2020. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka wizara ya afya imesema visa vipya 354 ni vya juu kuwahi kusajiliwa nchini humo chini ya kipindi cha saa 24.

Takriban wiki sita zimepita tangu kisa cha kwanza cha Covid 19 kuripotiwa nchini Afrika Kusini, na idadi ya maambukizi imekuwa ikiongezeka kila kukicha.

Hivi karibuniAfrika Kusini ilichukuwa mikakati mipya kupambana dhidi ya Corona katika magereza mbalimbali nchini humo, baada ya wafungwa 59 na wafanyakazi wa gereza 29 kuthibitishwa kuambukizwa katika kipindi cha majuma mawili.

Hofu ya kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona inaendelea kuwa janga la ulimwengu mzima na kila sekunde visa vipya vya maambukizi vinaripotiwa katika nchi mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.