Pata taarifa kuu
EU-BURUNDI-MASHAURIANO-UCHUMI

Mashauriano na EU: Burundi "yaridhika" hata kama

Mashauriano baina ya Umoja wa Ulaya (EU) na Burundi hayakufikia maelewano. Na huenda Umoja huo ukachukua hatua kali dhidi ya Burundi, Mashauriano hayo yalifanyika katika mji wa Brussels, nchini Ubelgiji, Jumanne wiki hii.

Willy Nyamitwe, mshauri wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Willy Nyamitwe, mshauri wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. © DR
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Bujumbura haikuweza kuushawishi Umoja wa Ulaya kuhusu nia yake ya kuheshimu haki za binadamu katika nchi hiyo inayokabiliwa na machafuko tangu kuchaguliwa upya kwa Rais Nkurunziza kwa awamu ya tatu.

Umoja wa Ulaya unaweza kuzuia ushirikiano wake wa mamilioni kadhaa ya Euro. Hata hivyo, serikali ya Bujumbura imesema kuwa "imeridhika" kuona mazungumzo na Umoja wa Ulaya yameanza upya.

Baada ya Umoja wa Ulaya kuchukua uamzi wa kusimamisha ushirikiano wake na Burundi mwezi Mei, kuna hatari ushirikiano huo upunguzwe "kwa misaada ya kibinadamu na kwa neema ya raia" kama serikali ya Bujumbura haitoi dhamana juu ya utawala bora na haki za binadamu.

Upande wa Burundi, wanabaini kwamba hawawezi kuchukua maamuzi ambayo yanaweza kuhatarisha uhuru wa taifa hilo. "Tulijaribu kuonyesha hali ilivyo kama wawakilishi wa serikali, na nchi yenye sheria na ambayo inapaswa, katika mazungumzo na washirika wake kutoa dhamana, na kuhakikishia washirika wake", amebaini Willy Nyamitwe, mshauri wa Rais Nkurunziza, akionyesha kwamba "wakati wowote iwapo sheria za nchi yake zitaruhusu, wako tayari kutekeleza ombi la Umoja wa Ulaya. "

Redio na mashirika yasiyo ya kiserikali

Wasiwasi ni kwenye vyama vya kiraia na vyombo vya habari vinavyofuatiliwa nchini Burundi. Willy Nyamitwe ameeleza mapendekezo yaliyotolewa kwa Umoja wa Ulaya. "Tulipendekeza kwamba kuhusiana na kusimamishwa kwa redio au mashirika yasiyo ya kiserikali, uchunguzi unaweza kuendeshwa kwa haraka ili kwa kipindi cha miezi miwili ijayo tuweza kuwa na jibu la wazi la kutoa", Nyamitwe amesema. Kwa maneno mengine, "kama mahakama itasema kwamba kweli vyombo hivi vya habari na mashirika yasio ya kiserikali havina hatia, vinaweza kuruhusiwa kuendelea na kazi zao."

Lakini mapendekezo hayo hayakuushawishi Umoja wa Ulaya. Kulingana na mkataba wa Cotonou, washirika wana muda wa miezi minne ili kukubaliana kuchukua uamzi wowote.

Cnared yaridhika

Kwa upande wake, upinzani wa kisiasa ulio uhamishoni, unakaribisha msimamo imara wa Umoja wa Ulaya.

"Tungependelea waharakie kuchukua hatua kali kwa sababu mauaji na mateso kwa raia yanayoendelea kushuhudiwa Burundi yanahitaji maamuzi ya nguvu, lakini tunakaribisha msimamo wa Umoja wa Ulaya", amesema Pacrace Cimpaye, naibu msemaji wa Cnared, upinzani wa kisiana ulio uhamishoni.

Hayo yanajiri wakati Jumatano wiki hii, watu wasiopungua watano waliuawa baada ya kushambulia kwa guruneti msafara wa polisi wilayani Cibitoke, moja ya kitovu cha maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza, Kaskazini mwa mji wa Bujumbura, kwa mujibu msemaji wa polisi ya Burundi, Pierre Nkurikiye. Madai hayo ya polisi yamekanushwa na mashahidi ambao wamesema kuwa raia waliouawa walikua hawana hatia yoyote, kwani walikutwa nyumbani kwao na kupigwa risasi kwa makusudi na polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.