Pata taarifa kuu
EU-BURUNDI-MASHAURIANO-UCHUMI

Serikali ya Burundi yashindwa kuishawishi EU

Baada ya siku nzima ya mashauriano kati ya Burundi na Umoja wa Ulaya mjini Brussels Jumanne hii, Umoja wa Ulaya haukutoshelezwa na mapendekezo yaliyotolewa na serikali ya Bujumbura juu ya kurekebisha makosa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo.

Makao makuu ya Tume ya Ulaya mjini Brussels. Mashauriano kati ya EU na Burundi yamefanyika katika faragha.
Makao makuu ya Tume ya Ulaya mjini Brussels. Mashauriano kati ya EU na Burundi yamefanyika katika faragha. © REUTERS/Francois Lenoirragha
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa utachukua hatua zinazofaa.

Tangazo la Umoja wa Ulaya limetolewa Jumanne hii saa 3:30 usiku, zaidi ya saa sita baada ya kuanza kwa majadiliano ambayo yalifanyika katika faragha.

Uamuzi uliyochukuliwa ni huu: misimamo "iliyotolewa na serilaki ya Bujumbura hairuhusu kurekebisha mapungufu ya ushirikiano muhimu ya Umoja wa Ulaya na Burundi". Kwa maneno mengine, serikali ya Bujumbura haikuweza kuweka wazi nia yake ya kurekebisha makosa ya ukiukaji wa haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia ambayoinatuhumiwa.

Au hata nia yake ya kukubali haraka kuelekea katika njia ya mazungumzo ya "dhati na umoja" yanayopendekezwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Vikwazo vya baadaye

Uamuzi huu umefungua njia ya vikwazo, na "hatua mwafaka" Brussels imesema, hadi kuvunjika kwa ushirikiano wake na Burundi. Lakini katika hatua hii, aina ya vikwazo haijatajwa. "Yote yategemea maendeleo ya mapendekezo yaliyotolewa na serikali ya Bujumbura", mwanadiplomasia mmoja wa Ulaya amesema. Mara baada tu ya vikwazo kutangazwa, vikwazo hivyo vitapitishwa na Baraza la Umoja wa Ulaya, pengine si mwanzoni mwa mwezi Januari.

Ni miezi kadhaa sasa Brussels ikiendelea kuongeza shinikizo kwa matumaini ya kulazimisha serikali ya Bujumbura kuanzisha mazungumzo na upinzani, bila hata hivyo mafanikio yoyote.

Katika taarifa iliyotolewa muda mfupi baadaye, serikali ya Burundi imesema kuwa "imeridhika na mkutano" kwa sababu umepelekea "kuanzishwa upya mazungumzo kati yake na Umoja wa Ulaya". "Ifhamike kwamba hakuna vikwazo vilivyotangazwa", serikali ya Burundi imepongeza huku ikisikitishwakuona Umoja wa Ulaya "imepuuzia" mapendekezo yaliyotolewa na Serikali. Hata hivyo serikali ya Bujumbura, imeahidi kuendelea kutekeleza ahadi zake "kuhusu uchunguzi unaofuatisha sheria na utaratibu wa mchakato wa mazungumzo ya kitaifa".

Bujumbura inazidi kutengwa

Kuzorota kwa mahusiano kati ya Umoja wa na serikali ya Bujumbura ina muda mrefu. Lakini kamwe katika mgogoro huu Brussels ilikua haijawahi kuonesha msimamo wake kama inavyofanya wakati huukutokana na kutokuwa na nia kwa serikali ya Bujumbura. Baada ya vikwazo Marekani dhidi ya maafisa wa wa usalam na ulinzi wa Burundi, baada ya uamuzi wa ICGLR, Jumuiya ya nchi za Maziwa Makuu kuondoa kwa muda makao yake makuu katika mji mkuu wa Burundi, hivyo hii ni hatua nyingine katika kutengwa kwa serikali ya Bujumbura kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.