Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SIASA

Salva Kiir aongezwa madaraka

Wabunge nchini Sudan Kusini wamebadilisha Katiba kumwongezea madaraka rais Salva Kiir.

Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir, Nairobi, Mei 11 mwaka 2014.
Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir, Nairobi, Mei 11 mwaka 2014. REUTERS/Thomas Mukoya/Pool
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya rais Kiir kuagiza kuongezwa kwa majimbo zaidi nchini humo.

Waziri wa Habari Michael Makuei amesema mabadiloko hayo yamefanyika ili kuhalalisha mamlaka ya rais kuongeza majimbo mapya.

Wachambuzi wa siasa za Sudan Kusini wanasema mabadiliko haya yanaweza kusabaisha kutotekelezwa kikamilifu kwa mkataba wa amani kati ya serikali na kiongozi wa waasi Riek Machar.

Itafahamika kwamba machafuko yanayoendelea kushuhudiwa nchini Sudan Kusini yamesababisha vifi vya maefu ya raia, huku raia wengi wakiyahama makazi yao.

Machafuko nchini humo yamechochewa kisiasa kufuatia hali ya kutoelewana kati ya Rais Salva Kiir na aliye kuwa makamu wake Riek Machar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.