Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MAPIGANO-USALAMA

Serikali ya Juba yawanyooshea kidole cha lawama waasi wa Riek Machar

Viongozi wa Sudan kusini wamedai kuwa wapiganaji wanaoongozwa na Riek Machar, wamewaua watu Ishirini na wawili  baada ya kurusha makombora kwenye jimbo la Jonglei.

Makubaliano yalifikiwa Sudan Kusini, kati ya vigogo wawili wanaopinzana Riek Machar (kushoto) na Salva Kiir (kulia), Agosti 26, 2015, mjini Juba.
Makubaliano yalifikiwa Sudan Kusini, kati ya vigogo wawili wanaopinzana Riek Machar (kushoto) na Salva Kiir (kulia), Agosti 26, 2015, mjini Juba. REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Inaarifiwa kuwa waasi wanaoongozwa na Riek Machar wameendesha mapamabano Jumanne asubuhi wiki hii katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Unity.

Msemaji rasmi wa jeshi la Sudan kusini, Kanali Philip Panyang Agwer, amethibitisha kuwa watu Ishirini na wawili wameuawa katika jimbo la Jonglei kutokana na mashambulizi yaliyotekelezwa na wapiganaji wanaomtii kiongozi wa waasi Riek Machar.

“Watu Ishirini na wawili wamepoteza maisha yao, pakiwemo na watoto na wanawake. Kitendo hiki cha mauaji kinakiuka mkataba wa amani”, amesema Kanali Philip Panyang Agwer.
 
“Leo Asubuhi waasi walishambulia jimbo la unity na inaonekana kama waasi hawana haja ya kuheshimu mkataba wa kusitisha mapigano”
, ameongeza Kanali Philip Panyang Agwer.

Hata hivyo waasi kupitia kwa msemaji wao, James Gadet Dak, amesema serikali ya Juba  inataka kuharibu mpango wa kuundwa serikali ya mpito kutokana na tuhuma zisiokuwa na msingi dhidi ya waasi

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.