Pata taarifa kuu

Wizara ya Ulinzi ya Urusi yadai 'kukomboa' vijiji sita mashariki mwa Ukraine

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema leo Jumamosi kuwa vikosi vyake vimedhibiti vijiji sita mashariki mwa Ukraine. Wizara hiyo imesema kwenye Telegraph kwamba wanajeshi "wamekomboa" vijiji vya Ukraine vya Borisivka, Ogirtseve, Pletenivka, Pylna na Strilecha katika mkoa wa Kharkiv, karibu na mpaka na Urusi, na pia kijiji cha Keramik katika mkoa wa Kharkiv.

Uharibifu unaofanywa na mashambulizi ya Urusi huko Kharkiv, Ukraine, Mei 10, 2024.
Uharibifu unaofanywa na mashambulizi ya Urusi huko Kharkiv, Ukraine, Mei 10, 2024. REUTERS - Vyacheslav Madiyevskyy
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi kadhaa ya Urusi yamesababisha vifo vya watu wawili na wengine 16 kujeruhiwa mashariki na kaskazini mashariki mwa Ukraine, haswa huko Kharkiv. Jeshi la Urusi linadai kutekwa kwa kijiji kipya, Otcheretyne, katika mkoa wa Donetsk.

Hivi karibuni Urusi ilifanya mashambulizi ya kuvuka mpaka kuelekea mji wa Kaskazini Mashariki mwa Ukraine wa Kharkiv, kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya ulinzi ya Ukraine na chanzo kimoja cha kijeshi.

Taarifa ya wizara ilidai kuzuia mashambulizi hayo lakini mapigano makali bado yanaendelea na kwamba Urusi imeanzisha mashambulizi ya angani karibu na eneo la mpaka.

Chanzo kingine cha ngazi ya juu ndani ya jeshi la Ukraine kilisema Urusi ilipiga hatua kadhaa umbali wa "kilometa moja" kuelekea Ukraine na inajaribu kuzuia mashambulizi ndani ya eneo la Urusi.

Ukraine ilifanikiwa kuvirejesha nyuma vikosi vya Urusi kutoka eneo kubwa la Kharkiv mwishoni mwa mwaka 2022, lakini mashambulizi ya Moscow sasa yamepamba moto, wakati vikosi vya Kyiv vikikabiliwa na uhaba wa silaha. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.