Pata taarifa kuu

Shambulio Moscow: Putin ashtumu 'Waislamu wenye itikadi kali' lakini bado anaishushia lawama Ukraine

Kwa mara ya kwanza, Rais wa Urusi Vladimir Putin ameshutumu "Waislamu wenye itikadi kali" kwa kuhusika na shambulio lililotokea katika viunga vya Moscow mnamo Machi 22. Shambulio hilo ambalo lilidaiwa na kundi la Islamic State, kwenye Ukumbi wa Jumba la tamasha la Crocus City Hall liliua takriban watu 139. Lakini kiongozi wa Urusi anaendelea kuishushia lawama Kyiv.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, katika ofisi yake ya Kremlin huko Moscow, Machi 23, 2024.
Rais wa Urusi Vladimir Putin, katika ofisi yake ya Kremlin huko Moscow, Machi 23, 2024. © Mikhail Metzel / AP
Matangazo ya kibiashara

Vladimir Putin amethibitisha siku ya Jumatatu Machi 25 kwamba shambulio la Ijumaa dhidi ya ukumbi wa tamasha karibu na Moscow, lililodaiwa na shirika la Islamic State (IS), lilifanywa na "Waislamu wenye itikadi kali" ambao, kulingana na Putin, kisha walijaribu kukimbilia Ukraine.

"Tunajua kwamba uhalifu (huu) ulifanywa na Waislam wenye itikadi kali wenye itikadi ambayo ulimwengu wa Kiislamu wenyewe umekuwa ukabiliana nayo kwa karne nyingi," ameuambia mkutano wa serikali, akitaja uhusiano huo kwa mara ya kwanza, siku tatu baada ya kundi la ISIS kudai kuhusika na shambulio hilo. “Tunafahamu ni nani aliyefanya unyama huu dhidi ya Urusi na watu wake. Tunachotaka kujua ni mfadhili,” ameongeza.

Kisha akarudia kwamba washambuliaji, baada ya shambulio hilo ambalo lilisababisha vifo vya watu 139, kulingana na ripoti mpya, walijaribu kukimbilia Ukraine kabla ya kukamatwa.

"Ni muhimu kujibu swali kwa nini magaidi, baada ya uhalifu wao, walijaribu kuondoka kwenda Ukraine? Nani alikuwa anawasubiri pale? Wale wanaounga mkono serikali ya Kyiv hawataki kuwa washirika wa ugaidi na wafuasi wa ugaidi, lakini maswali mengi yanaibuka," rais wa Urusi amesema.

“Nani anafaidika na hili? ", anauliza Vladimir Putin

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Bw. Putin na idara zake za usalama za FSB hawakutaja kuhusika kwa wanajihadi, kwa pamoja waliutaja uongozi wa Ukraine, madai ambayo yalikanusha vikali na Kyiv na nchi za Magharibi. Hata hivyo siku ya Jumatatu Machi 24, rais wa Urusi alidokeza tena kwamba shambulio hilo linaweza kuwa na uhusiano na Kyiv na wafuasi wake.

"Mara moja, mtu anajiuliza ni nani anayefaidika na hii? Ukatili huu unaweza kuwa sehemu mpya katika mfululizo wa majaribio ya wale ambao, tangu mwaka 2014, wamekuwa wakipigana na nchi yetu kupitia utawala wa huko Kyiv," amesema. "Na Wanazi, inajulikana, hawakuwahi kudharau kutumia njia chafu na zisizo za kibinadamu kufikia malengo yao," amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.