Pata taarifa kuu

Uanachama wa NATO wa Sweden: Putin "ameshindwa", Muungano una "nguvu" (Stoltenberg)

Kujiunga kwa Sweden katika Jumuiya ya Kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, ni tukio la "kihistoria" na inaonyesha kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin "ameshindwa" katika jaribio lake la kudhoofisha Muungano huo, Katibu Mkuu wake Jens Stoltenberg amesema leo Jumatatu Machi 11.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akizungumza katika Kongamano la NATO mjini Stockholm, Jumatano, Oktoba 25, 2023.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akizungumza katika Kongamano la NATO mjini Stockholm, Jumatano, Oktoba 25, 2023. AP - Jonas Ekstromer
Matangazo ya kibiashara

“Wakati Rais Putin alipoanzisha uvamizi wake dhidi ya (Ukraine) miaka miwili iliyopita, alitaka NATO ipungukiwe nguvu na kuwadhibiti majirani zake. Alitaka kuiangamiza Ukraine kama taifa huru, lakini alishindwa,” Katibu Mku wa NATO Jens Stoltenberg amesema.

"NATO ni kubwa na ina nguvu zaidi," ameongeza wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson katika makao makuu ya jumuiy hiyo huko Brussels, kulingana na shirika la habari la  AFP.

Wakati huo huo bendera ya Uswidi, ambayo imekuwa mwanachama wa 32 wa NATO, imepandishwa leo Jumatatu katika makao makuu ya NATO, kielelezo cha safari ndefu kwa nchi hii ya Scandinavia.

Sweden ilichagua, baada ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine mnamo Februari 24, 2022, kuachana na karne mbili za kutoegemea upande wowote na kutojihusisha na kijeshi, kujiunga na muungano mkuu wa kijeshi ulimwenguni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.