Pata taarifa kuu

Ufaransa: Wabunge na maseneta wafikia makubaliano kuhusu mswada wa uhamiaji

Wabunge na maseneta waliokutana katika kamati ya pamoja (CMP) wamefikia makubaliano mnamo Jumanne kuhusu mswada wa uhamiaji, kwa uungwaji mkono wa chama cha Rassemblement national (RN), baada ya masaa marefu na magumu ya mazungumzo.

Kiongozi wa wabunge wa chama cha  Les Républicains Olivier Marleix akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Bunge la taifa mnamo Desemba 19, 2023.
Le chef des députés Les Républicains Olivier Marleix s'adresse aux journalistes à l'Assemblée nationale le 19 décembre 2023. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

CMP, inayoundwa na maseneta saba na wabunge saba, ilianza kazi yake siku ya Jumatatu saa kumi na moja jioni kisha ikarejelea saa 10:30 asubuhi baada ya usiku wa mvutano, kutokana na kutoelewana kwa dakika za mwisho kuhusu suala la manufaa ya kijamii. Inabaki nakala hii kupitisha hatua ya kupiga kura katika mabunge yote mawili, kikao ambacho kimepangwa kufanyika leo jioni.

“Makubaliano yanafikiwa na Bunge kuhusu mswada wa uhamiaji. Hili ni jambo zuri: hatua zinazowalinda Wafaransa, uthabiti muhimu kwa wageni wahalifu, na hatua za haki kama vile mwisho (wa kihistoria) wa kuwazuilia watoto wadogo au kuhalalisha wafanyakazi, amejibu Gérald Darmanin kwenye mtandao wa X (zamai ikiitwa Twitter).

RN itapigia kura mswada

Kiongozi wa chama cha LR Eric Ciotti amethibitisha kwamba Warepublican "walilaimosha" nakala kuhusu uhamiaji kutoka Tume ya Pamoja (CMP) na akahakikisha kwamba wabunge wote 62 wa chama chake wataidhinisha. "Leo, ni Warepublican ambao, kutokana na kazi yao, kutokana na maoni yao, wamelazimisha nakala hii," kiongozi wa LR ametangaza mbele ya waandishi wa habari, ambaye aliona kuwa nakala hii ina "mabadiliko ya kweli".

Wabunge wa RN watapigia kura mswada wa uhamiaji "kama ulivyoafikiwa na kamati ya pamoja", ametangaza kiongozi wao Marine Le Pen, akikaribisha "sheria ya kuimarisha hali ya uhamiaji".

"Tunaweza kushangilia maendeleo ya kiitikadi, ushindi hata wa kiitikadi kwa chamacha RN, kwani kipaumbele cha kitaifa sasa kimewekwa katika sheria hii, hii ni kusema, faida waliyopewa Wafaransa juu ya wageni waliopo kwenye ardhi yetu kupata baadhi ya haki ambazo leo ziko chini ya masharti kwa wageni ambayo sio magumu kwa kweli kwa muono wetu, "ameongeza.

"Ni aibu kwa serikali"

Kinyume chake, wawakilishi waliochaguliwa wa mrengo wa kushoto hawakuwa na maneno makali ya kutosha kwa maelewano haya, wakizungumza juu ya "mgogoro wa maadili" au hata "kula njama na nadharia za haki kali", muswada huo ukiidhinisha kanuni ya "upendeleo wa kitaifa” uliotetewa kwa muda mrefu na chama cha RN na mbele yake chama cha Front national.

Kiongozi wa wabunge wa kisoshalisti Boris Vallaud ameamua kwamba makubaliano yaliyofikiwa ni "wakati wa kufedheheka kwa serikali." "Ni aibu kabisa na ninatumai kuwa katika safu ya wengi kutakuwa na wanawake na wanaume wenye ujasiri na kanuni. kukataa maelewano haya,” ameongeza mbunge huyo, akiamini kwamba “hakuna mtu aliyelazimika kujitoa hivyo kwa Warepublican na kwa mrendo wa kulia wenye msimamo mkali.”

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.