Pata taarifa kuu

Chama cha kihafidhina chashinda uchaguzi nchini Uhispania

Nairobi – Nchini Uhispania, chama cha upinzani cha kihafidhina cha Popular Party kimeibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu wa dharura uliofanyika hapo jana Jumapili.

Kiongozi wa chama hicho Alberto Núñez Feijóo, ametangaza kuwa chama chake kimeibuka mshindi
Kiongozi wa chama hicho Alberto Núñez Feijóo, ametangaza kuwa chama chake kimeibuka mshindi AFP - JAVIER SORIANO
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa chama hicho Alberto Núñez Feijóo, ametangaza kuwa chama chake kimeibuka mshindi, lakini kimeshindwa kupata idadi kubwa ya viti bungeni ili kuunda serikali peke yake.

Baada ya asilimia 99.5 ya kura kuhesabiwa, chama cha PP kimepata viti 136 huku kile cha Kisosholisti cha Pedro Sánchez, kikipata viti 122 katika bunge hilo la viti 350.

Matokeo haya yanaonesha kuwa, hakuna chama kilichopata viti 176 ili kuunda serikali bila ya kushirikisha vyama vingine.

Alberto Nunez Feijoo, ambaye chama chake kimepata viti vingi, amesema atajaribu kuunda serikali, huku wachambuzi wa siasa za nchi hiyo wakisema Waziri Mkuu Sanchez huenda akafanikiwa kuunda serikali kwa sababu ya kuwa madarakani kwa miaka mitano iliyopita na kuwa na uhusiano mzuri na vyama vya Basque na vuguvugu la Catalan.

Uchaguzi huu umefanyika baada ya mwezi Mei, chama cha Kisosholisti kushindwa kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na majimbo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.