Pata taarifa kuu

Elon Musk atishia kuishtaki Meta baada ya uzinduzi program mpya inayoitwa Threads

Nairobi – Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Elon Musk, kupitia wakili wake, ametishia kuishtaki Meta baada ya mtandao wake tanzu wa Instagram kuzindua program mpya inayoitwa Threads, inayolenga kutoa ushindani na kuwa mbadala wa Twitter.

 Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Elon Musk, kupitia wakili wake, ametishia kuishtaki Meta baada ya mtandao wake tanzu wa Instagram kuzindua program mpya inayoitwa Threads
Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Elon Musk, kupitia wakili wake, ametishia kuishtaki Meta baada ya mtandao wake tanzu wa Instagram kuzindua program mpya inayoitwa Threads © AP/Richard Drew
Matangazo ya kibiashara

Katika barua iliyotumwa kwa mkurugenzi wa Meta, Mark Zuckerberg, na kuchapishwa mitandaoni hapo jana, wakili wa Musk, Alex Spiro, ameituhumu kampuni hiyo kwa kutumia siri za kibiashara za mtandao Wake pamoja na haki miliki nyingine.

Barua inaituhumu Meta kwa kuajiri mamia ya wafanyakazi wa Twitter waliofutwa kazi na ambao walikuwa bado wananyaraka na uwezo wa kutumia tarifa za kibiashara za mtandao huo pamoja na tarifa nyingine za siri.

Threads ilizinduliwa kama programu mbadala itakayotoa ushindani kwa Twitter, ambayo tangu Musk ainunue amekuwa akifanya mabadiliko ambayo watumiaji Wake wengi wameyakosoa na wengine hata kujiondoa kutumia mtandao huo.

Saa chache tangu kuzinduliwa kwake, Threads ilishuhudia ikipata wafuasi zaidi ya milioni 30 katika muda mchache ambapo sasa unapatikana kwenye nchi zaidi ya 100 duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.