Pata taarifa kuu
SIASA-UCHAGUZI

Ugiriki: Tsipras ajiuzulu kama kiongozi wa Syriza baada ya kushindwa katika uchaguzi

Wakati wa hotuba ya mchana huko Athens mnamo Juni 29, Waziri Mkuu wa zamani Alexis Tsipras ametangaza kujiuzulu. Uamuzi huu wa kuachia ngazi katika uongozi wa chama cha Syriza, chama cha kwanza cha upinzani nchini Ugiriki, unakuja siku chache baada ya kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi wa wabunge. 

Alexis Tsipras, kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto cha Syriza, baada ya hotuba yake katika ukumbi wa mikutano wa Zappeio huko Athens, Ugiriki, Alhamisi, Juni 29, 2023.
Alexis Tsipras, kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto cha Syriza, baada ya hotuba yake katika ukumbi wa mikutano wa Zappeio huko Athens, Ugiriki, Alhamisi, Juni 29, 2023. AP - Petros Giannakouris
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Athenes, Joël Bronner

Syriza, chama cha mrengo wa kushoto kilichotawala nchi kati ya 2015 na 2019, kwa hakika kilimaliza chaguzi hizi kwa pointi 22 nyuma ya chama cha mrengo wa kulia cha New Democracy, kuthibitisha matokeo yaliyopatikana mwezi mmoja awali, wakati wa kura ya kwanza.

Suti ya bluu na shati nyeupe, ni kwa utulivu fulani ambapo Alexis Tsipras alitangaza kuachia ngazi kama kiongozi Syriza, chama cha kwanza cha upinzani nchini Ugiriki. Kwa kufanya hivyo, anatoa mafunzo kutokana na kushindwa kwa uchaguzi wa hivi majuzi dhidi ya mrengo wa kulia unaoondoka, na kuchaguliwa tena kwa ushindi Jumapili iliyopita kwa 40% ya kura, ambapo chama cha Syriza kilipata tu zaidi ya 17%.

"Kama nilivyosema baada ya uchaguzi, tuko mwisho wa mzunguko wa kihistoria," Alexis Tsipras amesema. Kwa hivyo wakati umefika wa kufungua kwa pamoja mzunguko mpya. Ni lazima tujihusishe katika mchakato wa upyaji wa kina na uundaji upya, unaojumuisha wanachama na marafiki wote wa chama. Syriza mpya ni kipaumbele cha haraka. Ninaelewa haja ya wimbi jipya la Syriza na nimeamua kujiweka kando ili lipite. »

Ukimsikiliza Waziri Mkuu wa zamani, ambaye alifuatilia tena historia ya Syriza, "chama kidogo" kilichoingia madarakani kati ya mwaka 2015 na mwaka 2019, kuondoka kwake kama kiongiz wa chama hicho kunapaswa kuwezesha "Syriza mpya" kuandika sura inayofuata ya historia yake ya kisiasa. huko Ugiriki. Historia mpya ambayo Alexis Tsipras hatakuwa tena mhusika mkuu wakati huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.