Pata taarifa kuu

Urusi inasema imezuia shambulio kubwa kutoka Ukraine

NAIROBI – Wizara ya Ulinzi nchini Urusi, inasema imezuia shambulio kubwa kutoka Ukraine, na kuwauwa wanajeshi wake 250.

Urusi imedai kuzuia shambulio kubwa kutoka nchini Ukraine
Urusi imedai kuzuia shambulio kubwa kutoka nchini Ukraine REUTERS - VIACHESLAV RATYNSKYI
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii hata hivyo, haithabitishwa lakini pia, Ukraine haijazungumzia madai hayo ya serikali ya Urusi.

Wizara ya ulinzi ya Urusi inasema, wanajeshi wa Ukraine walijaribu kutekeleza shambulio kubwa katika jimbo la Donetsk kwa kutumia magari ya kijeshi na vikosi vyake vya ardhini, bila mafanikio.

Aidha, Moscow inadai kuwa imeharibu magari 16 ya kijeshi pamoja na vifaa vingine, vilivyokuwa vinatumliwa na wanajeshi wa Ukraine.

Ripoti hii kutoka Urusi, imekuja baada ya wiki iliyopita, Ukraine kusema kuwa ilikuwa tayari kutekeleza mashambulio katika majimbo yake yaliyochukuliwa na wanajeshi wa Urusi.

Hata hivyo, baada ya kauli hiyo ya Ukraine haijafahamika iwapo operesheni hiyo imeanza, huku ikionya kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa taarifa za kupotosha inazosema, zinaweza kumsaidia adui.

Donetsk ni miongoni mwa majimbo yaliyochukuliwa na Urusi, pamoja na Luhansk, Zaporizhia na Kherson baada ya kuivamia Ukraine mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.