Pata taarifa kuu
SIASA-UCHAGUZI

Erdogan asalia kuwa kiongozi wa Uturuki baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa urais

Rais Recep Tayyip Erdogan ameshinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Uturuki Jumapili hii, Mei 28. Amechaguliwa tena kwa miaka mitano. Miradi mingi inamsubiri.

Rais wa Uturuki Erdogan akihutubia umati wa wafuasi wake waliokusanyika nje ya ikulu ya rais mjini Ankara baada ya ushindi wake, Mei 29, 2023.
Rais wa Uturuki Erdogan akihutubia umati wa wafuasi wake waliokusanyika nje ya ikulu ya rais mjini Ankara baada ya ushindi wake, Mei 29, 2023. © UMIT BEKTAS / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Recep Tayyip Erdogan anasalia kuwa kiongozi wa Uturuki kwa miaka mingine mitano. Licha ya kuwa na hamu kubwa ya mabadiliko kutoka kwa sehemu ya wapiga kura, mkuu huyo wa nchi mwenye umri wa miaka 69 alianza kama mshindi katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais akiongoza kwa pointi tano katika duru ya kwanza iliyofanyika Mei 14 , ambapo amepata 49.5% ya kura. Akiwa madarakani kwa miaka ishirini, ameshinda kwa 52.1% ya kura, dhidi ya 47.9% ya mpinzani wake Kemal Kiliçdaroglu baada ya kuhesabu karibu 99.7% ya kura, na kutangazwa mshindi na tume ya uchaguzi.

Ushindi huo haukuwa mpana kama ilivyotarajiwa na kambi ya rais. Na baadhi ya wafuasi wa chama cha AKP katika ngome kuu ya chama hicho wanasema wanashangazwa kuona katika duru hii ya pil kumekuwa na tofauti ya pointi kati ya Kemal Kiliçdaroglu na Recep Tayyip Erdogan ikilinganishwa na tofauti ya pointi 5 katika duru ya kwanza, anaripoti mwandishi wetu maalum huko Istanbul, Daniel Vallot. Wafuasi wengi wa Erdogan walikuwa wakitarajia zaidi ya 60% ya kura. "Lakini jambo kuu, ni kuridhika ushidi huu wa chama cha AKP, ni kwamba ushindi unapatikana na kwamba rais wa Uturuki anaweza kuendeleza kazi iaiyoanza miaka 20 tu iliyopita", amesema mmoja wa wafuasi wa chama cha rais.

'Kumpinga Erdogan ni sawa na kuipinga serikali'

Mambo matatu yanaweza kutoa matumaini kwa mabadiliko, Samim Akgonül, mkurugenzi wa idara ya masomo ya Kituruki katika Chuo Kikuu cha Strasbourg ameiambia RFI. Kwanza, uchakavu wa madaraka baada ya miaka 20 kama mkuu wa nchi. Kisha, mgogoro wa kiuchumi ambao umedumu kwa miaka miwili na mfumuko wa bei na umaskini wa unaowakabili raia. Kiwango rasmi cha mfumuko wa bei kilikuwa zaidi ya 40% kwa mwaka mmoja baada ya kuzidi 85% katika msimu wa wa joto, matokeo ya kushuka kwa viwango vya riba vilivyotarajiwa na Rais Erdogan. 

Wakati huo huo rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa upande wake amesema anatumai "kuimarika zaidi kwa ushirikiano wa kimkakati" kati ya Kiev na Ankara, "pamoja na kuimarishwa kwa ushirikiano wetu kwa usalama na utulivu wa Ulaya. Uturuki ina jukumu la upatanishi katika mzozo wa Urusi na Ukraine. 

Naye Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz pia amempongeza Recep Tayyip Erdogan, akiita Uturuki na Ujerumani "washirika wa karibu", ambao "watu na uchumi wameunganishwa". "Ninatarajia kuendelea kufanya kazi pamoja kama washirika wa NATO katika masuala ya nchi mbili na changamoto za kimataifa," Rais wa Marekani Joe Biden ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter. "Ufaransa na Uturuki zina changamoto kubwa ambazo nchi hizi zinatakiwa kukabiliana nazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.