Pata taarifa kuu
ULINZI-DIPLOMASIA

Urusi yaanza kuhamisha silaha za nyuklia kwa Belarus, Lukashenko atangaza

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amesema Alhamisi Mei 25 kwamba Urusi imeanza kuhamisha silaha za nyuklia kwa nchi yake, na kuhitimisha uwekaji uliotangazwa mwezi Machi na Vladimir Putin.

Vladimir Putin na Alexander Lukashenko Jumamosi Juni 5, 2022 huko St. Petersburg.
Vladimir Putin na Alexander Lukashenko Jumamosi Juni 5, 2022 huko St. Petersburg. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Uhamisho wa silaha za nyuklia umeanza, tayari umeanza," amesema Alexander Lukashenko, akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari wa Urusi katika matangazo ya video yaliyorushwa hewani na kito cha Telegram kisicho rasmi cha ofisi ya urais wa Belarus, Pul Pervogo. Rais wa Belarus, ambaye alikuwa Moscow Alhamisi hii, Mei 25 kwa mkutano wa kilele wa kikanda, hata hivyo hakuweza kuashiria ikiwa silaha zinazohusika zilikuwa tayari nchini mwake. Ameeleza kuwa Vladimir Putin alimwambia siku moja kabla kwamba alikuwa ametia saini sheria ya kuruhusu uhamisho huo.

Rais wa Urusi alitangaza mnamo Machi 25 kwamba Moscow itapeleka silaha za nyuklia kwenye ardhi ya Belarus, nchi iliyoko kwenye malango ya Umoja wa Ulaya, na kuchochea hofu ya kuongezeka kwa mzozo nchini Ukraine. Tangazo hilo limezua ukosoaji kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, hasa nchi za magharibi, hasa kwa vile kiongozi huyo wa Urusi tangu kuanza kwa shambulio lake dhidi ya jirani yake  Ukraine mnamo Februari 2022 aliibua uwezekano wa kutumia silaha za atomiki.

'Tishio jipya kwa Ulaya yote'

Mpinzani wa Belarus aliye uhamishoni, Svetalana Tikhanovskaya, ameshutumu tishio kwa bara zima la Ulaya. "Haihatarishi tu maisha ya Wabelarus, lakini pia inaleta tishio jipya kwa Ukraine, kwa Ulaya yote," ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter. "Inapokuja suala la silaha za kiteknolojia za nyuklia, nyingi zina nguvu kama ile iliyoua watu 140,000 huko Hiroshima," ameongeza. Silaha za nyuklia zinazoitwa "mbinu" zinaweza kusababisha uharibifu mkubwa, lakini eneo lao la uharibifu ni mdogo zaidi kuliko zile za nyuklia zinazoitwa "mkakati".

Mapema mwezi Aprili, Urusi ilisema imeanza kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Belarus katika matumizi ya silaha hizo za nyuklia. Kwa kuongezea, Vladimir Putin hapo awali aliashiria kuwa ndege kumi tayari zimewekwa tayari huko Belarus kwa matumizi ya silaha hizo na kwamba ghala maalum litakamilika ifikapo Julai 1.

Belarus haishiriki moja kwa moja katika vita nchini Ukraine, lakini iliruhusu jeshi la Urusi kutumia ardhi yake ili liweze kuzindua shambulio lake mnamo mwezi Februari 2022.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.