Pata taarifa kuu

Ukraine: Wagner yatangaza kujiondoa Bakhmout ifikapo Juni 1

Kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner linapanga kukabidhi ngome zake kwa jeshi la Urusi ifikapo mwisho wa mwezi huu, ingawa Ukraine bado inakanusha kuchukualiwa kwa mji wa Bakhmut.

Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, anatoa tangao akiwa pamoja na wapiganaji wa Wagner, katika picha hii kutoka video iliyotolewa Mei 5, 2023.
Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, anatoa tangao akiwa pamoja na wapiganaji wa Wagner, katika picha hii kutoka video iliyotolewa Mei 5, 2023. via REUTERS - PRESS SERVICE OF "CONCORD\
Matangazo ya kibiashara

Kutekwa kwa mji wa Bakhmut kulitangazwa Jumamosi Mei 20 na kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner. Hata hivyo, Ukraine inaendelea kudai kuwa bado inadhibiti majengo machache katika jiji hilo lililoharibiwa kwa kiasi kikubwa, na juu ya yote kusonga mbele katika vitongoji vyake kwa kushambulia pande za Urusi. Bado, kiongozi wa Wagner, Yevgeny Prigozhin, amebaini kwamba wapiganaji wake wataondoka katika mji huo ifikapo Juni 1, mara tu uhamisho wa ngome zao kwa jeshi la Urusi utakapokamilika.

"Katika viunga vya magharibi (ya Bakhmut), safu za ulinzi zipo. Kwa hivyo ikundi la Wagner litaondoka Artiomovsk [jina la Bakhmut] kati ya Mei 25 na Juni 1, "amesema Yevgeny Prigozhin leo Jumatatu katika rekodi ya sauti iliyorushwa na idara yake ya vyombo vya habari.

'Mapigano yanaendelea'

Kiongozi wa kundi la wanamgambo la Wagner ameshambulia tena uongozi wa kijeshi wa Urusi, ambao ana mgogoro nao, akiwashutumu wale waliohusika kuwanyima wapiganaji wake risasi na kuwa mbali sana na uwanja wa vita. "Ikiwa hakuna vitengo vya kutosha vya Wizara ya Ulinzi (kuchukua Bakhmut), kuna maelfu ya majenerali (kufanya hivyo), itabidi kuunda kikosi cha majenerali, kuwapa bunduki za aina mbalimbali, na kila kitu kitakuwa sawa, "amesema leo Jumatatu.

Kyiv haijathibitisha kupoteza kwa mji wa Bakhmut. Siku ya Jumapili kamanda wa vikosi vya ardhini vya Ukraine, Oleksandre Syrsky, alisema kwamba wanajeshi wake hawakudhibiti tena sehemu "isiyo na maana" ya mji huo, lakini wanaendelea kusonga mbele kwenye ukingo wake. Siku ya Jumatatu, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Ganna Maliar aliwatolewa wito wanajeshi wa Ukraine waliotumwa Bakhmut "kudhibiti baadhi ya majengo", akiongeza kwenye Telegram kwamba "mapambano ya pande zote, kaskazini na kusini, yanaendelea". "Mapigano yanaendelea," aliongeza.

Bi. Maliar pia alikaribisha mafanikio ya kimbinu, kulingana na maneno yake, ya ulinzi usiokoma wa jeshi la Ukraine kwa mji huu ambao sasa umeharibiwa na vita.

Kwa hakika, kulingana na wachambuzi na Kiev, vikosi vya Urusi vimejitolea watu na vifaa vingi kili kudhibiti Bakhmut, askari ambao Warusi wanaweza kukosa wakati Ukraine itakapozindua mashambulizi yake katika maeneo yaliyokaliwa. "Ulinzi wa Bakhmut unatimiza malengo yake ya kijeshi," Bi Maliar amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.