Pata taarifa kuu

EU yaionya Moscow kuhusu kulipiza kisasi madai ya njama ya kumuua Putin

NAIROBI – Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, ameionya Moscow dhidi ya kutumia madai ya shambulio la ndege zisizo na rubani lililolenga Kremlin, ili kukomaza vita vyake nchini Ukraine.

Mkuu wa sera za kigeni za EU Josep Borrell.
Mkuu wa sera za kigeni za EU Josep Borrell. AP - Virginia Mayo
Matangazo ya kibiashara

Borrell amewaambia waandishi wa habari akiwa jijini Brussels Ubelgiji kuhusu hofu hii.

Hili ndilo linalotutia wasiwasi, hii inaweza kutumika kuhalalisha usajili zaidi wa watu, askari zaidi, mashambulizi zaidi dhidi ya Ukraine, amesema Borrell.

Jumatano, Mei 3, Moscow ilisema vitengo vya kupambana na ndege viliiangusha ndege hizo zisizo na rubani, ikidai shambulio hilo lilikuwa jaribio la kumuua Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye huwa halali katika Ikulu ya Kremlin.

Nilimsikiliza Rais Volodymyr Zelensky alisema waziwazi Ukraine haihusiki na mashambulizi hayo, kwamba wanailinda nchi yao, lakini wanapigana kwenye ardhi yao, kwamba hawashambulii ardhi ya Urusi, Amesema Borrell.

Rais wa zamani wa Urusi, Dmitry Medvedev, kwenye mtandao wa Twitter, amekosoa matamshi yake Borrell, akisema shambulio hili litaongeza mzozo uliopo.

Hivi ndivyo tu Washington na viongozi wengi huko Brussels wanataka, Medvedev amesema.

Ikulu ya White House, Jumatano ilisema kwamba Kremlin inadanganya kwa kuishutumu Washington kwa kuiongoza Ukraine kuanzisha shambulio hilo linalodaiwa kuwa la ndege zisizo na rubani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.