Pata taarifa kuu

Naibu waziri mkuu wa Uingereza ajiuzulu

NAIROBI – Naibu waziri mkuu wa Uingereza Dominic Raab, mnamo Aprili 21, ametangaza kujiuzulu, baada ya madai ya uonevu dhidi yake, kuthibitishwa katika ripoti, hatua ambayo huenda ikatikisa chama cha Conservative.

Naibu waziri mkuu wa Uingereza, Dominic Raab
Naibu waziri mkuu wa Uingereza, Dominic Raab © Chris J Ratcliffe/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Kujiuzulu kwa Raab, ni pigo kwa waziri mkuu Rishi Sunak, ikizingatiwa kuwa ni wiki mbili zimesalia kabla ya uchaguzi wa wabunge kuandaliwa.

Sunak pia anakabiliwa kibarua kigumu cha kuweka chama chake kuwa imara ili kisipoteze kwa upinzani, wakati huu uchaguzi mkuu ukitarajiwa kuandaliwa mwaka ujao.

Mnamo mwaka 2020, Raab aliahidi kujiuzulu iwapo madai yoyote dhidi yake yangesalia.

"Ingawa ninahisi kuwa na wajibu wa kukubali matokeo ya uchunguzi huo, ilitupilia mbali madai yote isipokuwa mawili yaliyotolewa dhidi yangu, pia ninaamini kuwa matokeo yake mawili mabaya yana dosari na yanaweka mfano wa hatari kwa mwenendo wa serikali nzuri." aliandika katika barua ya kujiuzulu.

Raab pia amejiuzulu kutoka kwa wadhifa wa waziri wa haki, ambapo alikuwa anakabiliana na mrundiko wa kesi za uhalifu, kutokana na ufadhili mdogo na Uviko 19.

Kama mtumishi wa umma, Raab, amewahi kuhudumu kama Waziri wa mchakato wa Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya maarufu Brexit, alihudumu kama waziri wa mambo ya nje, pia alimrithi Liz Truss kwa kipindi kifupi mwaka 2022, wakati aliahidi kurejesha maadili na uwajibikaji katika serikali, kutokana na msukomsuko uliokumba serikali ya waziri mkuu wa zamani Boris Johnson

 

Amekanusha madai hayo

Wakili Raab, amekanusha madai ya uonevu kwa wafanyakazi wake na katika barua yake amesisitiza, mawaziri wanapaswa kuruhusiwa kufanya uangalizi wa moja kwa moja ili kuwawajibisha viongozi wanaowawakilisha raia wa Uingereza.

Mwezi Novemba, Sunak alimteua wakili wa Adam Tolley kuangazia madai haya dhidi ya Raab, na siku ya Alhamisi, Sunak alipokezwa ripoti hiyo.

Ripoti hiyo inasubiriwa kuchapishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.