Pata taarifa kuu

Uuzaji wa mafuta ya Urusi wakabiliana na vikwazo vya Magharibi

Jumla ya usafirishaji wa mafuta iliongezeka mnamo Machi kutoka mapipa 600,000 kwa siku hadi mapipa milioni 8.1 kwa siku.

Meli kubwa ya mafuta huko Novorossiysk, mojawapo ya vituo vikubwa zaidi vya bidhaa za petroli kusini mwa Urusi, Jumanne, Oktoba 11, 2022.
Meli kubwa ya mafuta huko Novorossiysk, mojawapo ya vituo vikubwa zaidi vya bidhaa za petroli kusini mwa Urusi, Jumanne, Oktoba 11, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Licha ya mfululizo wa vikwazo kutoka kwa Umoja wa Ulaya na kundi la mataifa 7 yaliyostawi zaidi kiviwanda (G7), mauzo ya mafuta ya Urusi yanaendelea kujidhatiti na yalifikia hata kiwango chake cha juu zaidi katika miaka mitatu mwezi Machi, lakini fedha wanazopata Moscow ni ziko chini ikilinganishwa na mwaka jana, kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA) iliyotolewa Ijumaa.

Jumla ya usafirishaji wa mafuta uliongezeka mwezi Machi kutoka mapipa 600,000 kwa siku hadi mapipa milioni 8.1 kwa siku, ikiwa ni pamoja na bidhaa za petroli iliyosafishwa, ambayo ilipanda kutoka mapipa 450,000 kwa siku hadi mapipa milioni 3.1 kwa siku.

"Usafirishaji wa mafuta ya Urusi mwezi Machi ulipanda hadi kiwango cha juu zaidi tangu mwezi Aprili 2020 kutokana na kuongezeka kwa mtiririko wa bidhaa ambao ulirejea katika viwango vilivyoonekana mara ya mwisho kabla ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine," inabainisha AIE, yenye makao yake mjini Paris, katika toleo lake la kila mwezi la hivi punde.

Matokeo yake, "makadirio ya mapato yaliongezeka mwezi Machi kutoka dola bilioni 1 hadi bilioni 12.7", lakini yamesalia chini kwa 43% kuliko mwaka mmoja uliopita, inabainisha IEA.

Licha ya vikwazo vya kimataifa vinavyolenga mafuta yake, Urusi inajitahidi kuelekeza mauzo yake ya hydrocarbon ya gesi kwa nchi zingine, kama vile India.

"Urusi ilikuwa msambazaji mkuu wa bidhaa ghafi nchini India mwezi Februari kwa mwezi wa nane mfululizo ikiwa na sehemu ya karibu 38%," shirika la mauzo ya mafuta la OPEC lilisema siku ya Alhamisi, likinukuu data kutoka Kpler, kampuni ya uchambuzi inayobobea katika malighafi.

Baada ya vikwazo vilivyowekwa tangu Desemba 5 dhidi ya mafuta yasiyosafishwa ya Urusi, vikwazo vya pili vya EU juu ya ununuzi wa bidhaa za petroli za Urusi kwa njia ya bahari, pamoja na bei ya juu ya bidhaa hizi zinazotumiwa na nchi za G7 vimeanza kutumika.

Katika kulipiza kisasi vikwazo hivi vilivyowekwa kujibu hujuma ya Moscow dhidi ya Ukraine iliyozinduliwa mwezi Februari 2022, Urusi ilikuwa imeonya mnamo Februari 10 kwamba itapunguza uzalishaji wake kwa mapipa 500,000 kwa siku, bila hata hivyo kufikia lengo hili mwezi Machi.

"Uzalishaji ghafi wa Urusi ulipungua kutoka takriban mapipa 290,000 kwa siku mwezi Machi hadi mapipa milioni 9.58 kwa siku, na kukosa lengo lake la kupunguza (...) huku nchi hiyo ikionekana kupeleka mapipa yake kwa washirika wapya licha ya vikwazo vya EU," imesema IEA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.