Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Kyiv yataka Urusi ijiondoe kutoka kwa 'kila mita ya mraba' ya Ukraine

Mkuu wa diplomasia ya Ukraine Dmytro Kouleba siku ya Jumanne aliitaka Moscow kujiondoa kutoka "kila mita ya mraba" ya Ukraine, akisisitiza kwamba hakuwezi kuwa na amani na Urusi 'kwa hali yoyote'.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa ziara yake huko Kherson, Ukraine, Jumatatu, Novemba 14, 2022.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa ziara yake huko Kherson, Ukraine, Jumatatu, Novemba 14, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

"Nataka kuwa wazi kabisa, Urusi lazima ijitoe katika kila mita ya mraba ya eneo la Ukraine. Hakuwezi kuwa na maelewano kuhusu maana ya neno kujiondoa," alisema Kouleba, ambaye alikuwa akizungumza katika mjadala wa jukwaa la "amani nchini Ukraine" chini ya mwamvuli wa Marekani.

"Katika vita hivi, tunatetea ulimwengu wa kidemokrasia kwa ujumla," aliongeza. "Hakuna nchi nyingine inayotaka amani zaidi ya Ukraine. Lakini amani kwa bei yoyote ni udanganyifu." Rais wa Ukraine Volodymyr alipaswa kushiriki katika kongamano hili lililoandaliwa kando ya Mkutano wa Kilele wa Demokrasia lakini akaomba radhi na nafasi yake ikachukuliwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje.

Hivi majuzi China iliwasilisha mapendekezo ya kumaliza vita nchini Ukraine, ambayo yalipokelewa kwa shingo upande na nchi za Magharibi, ambazo zinasisitiza juu ya mamlaka ya Ukraine na uadilifu wa eneo lake. Mwenyeji wa mkutano huo wa mtandaoni, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, alionya kuhusu "mtego wa kijinga" unaoletwa na baadhi ya mipango ya amani ambayo hakutaja.

"Nadhani mnapaswa kuwa waangalifu na kile kinachoweza kuonekana kama kutuliza hali lakini inaweza kugeuka kuwa mtego wa kijinga," alisema, akimaanisha kwa mfano usitishaji wa mapigano ambao unaweza "kuzuia mzozo" na kuruhusu Urusib"kuunganisha maslahi yake na kujipanga upya".

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna alisisitiza juu ya ukweli kwamba "haki lazima itendeke", na kusisitiza katika suala hili kwamba waranti wa kukamatwa uliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inayomlenga Rais wa Urusi Vladimir Putin iliwakilisha "hatua kubwa" katika mapambano dhidi ya kutokujali.

Pia alitoa wito kwa nchi za Ulaya kuheshimu wajibu wao katika muktadha huu na kumfikisha rais wa Urusi kwa ICC ikiwa ataingia Umoja wa Ulaya. Hungary imedokeza kuwa haitamkabidhi bwana Putin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.