Pata taarifa kuu

Moldova yavunja kundi 'lililoundwa na Moscow' ili kuhatarisha usalama wa nchi

Polisi wa Moldova wametangaza Jumapili Machi 12, saa chache kabla ya maandamano dhidi ya serikali, kwamba imewakamata wanachama wa mtandao "uliopangwa na Moscow" kwa lengo la kuharibu nchi hii ndogo ya Umoja wa Kisovyeti wa zamani.

Askari wa Moldova wakati wa mazoezi mnamo mwaka wa 2011.
Askari wa Moldova wakati wa mazoezi mnamo mwaka wa 2011. © Wikimedia Commons CC BY 2.0 Staff Sgt. Brendan Stephens/US Army Europe
Matangazo ya kibiashara

Baada ya upekuzi Jumamosi jioni, watu 25 walihojiwa na wachunguzi na saba kati yao waliwekwa chini ya ulinzi mkali, mkuu wa polisi Viorel Cernautean amesema katika mkutano na waandishi wa habari, shirika la habari la AFPlimeripoti.

Afisa mmoja aliweza kujipenyeza katika kundi linaloongozwa na Mrusi-Moldavian, amesema, akibaini "saa kumi" ya rekodi za video na sauti ambavyo alikuwa navyo. "Watu wametoka Urusi wakiwa na jukumu maalum la mafunzo," ameongeza afisa huyo. Mamlaka ya Moldova imeeleza kwamba walichukua hatua baada ya "kupokea taarifa juu kufanyika kwa vitendo vya uharibifu kwenye nchi yetu kupitia maandamano, ambavyo viliandaliwa na idara maalum za Urusi ".

Chama cha kiongozi anayeiunga mkono Urusi Ilhan Shor kilikusanya wanajeshi wake tena katika wiki za hivi karibuni dhidi ya serikali inayounga mkono Ulaya, huku kukiwa na mvutano mkubwa kati ya Moscow na Chisinau. Chama hiki kilifanya maandamano kadhaa, ambapo kilishukiwa kuwalipa washiriki. Maandamano mapya yamepangwa kufanyika Jumapili hii mchana katika mji mkuu wa Chisinau.

Ikulu ya White House ilishutumu Urusi siku ya Ijumaa kwa kutaka kuhatarisha usalama wa nchi hiyo inayozungumza Kiromania yenye wakazi milioni 2.6 jirani na Ukraine, kwa lengo la kuweka serikali ambayo itatekeleza azma yake. Marekani ilisema imeimarisha mpango wake kupeana taarifa na viongozi wa Moldova ili "waweze kuchunguza zaidi" na "kuzuia mipango ya Urusi".

Moldova, iliyokuwa katika eneo la ushawishi la Urusi, sasa inatawaliwa na mamlaka iliyogeukia kwa uthabiti ushirikiano wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.