Pata taarifa kuu

Silaha bandia zatumika katika vita vya Ukraine

NAIROBI – Kampuni moja nchini Jamuhuri ya Czech, inayotengeneza silaha za plastic, ikiwemo roketi na vifaru, imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya vifaa hivyo tangu Urusi ivamie Ukraine, mwanzoni mwa mwaka jana.

Wanajeshi wa Ukraine wameendelea kukabiliana na mamluki wa Urusi Wagner kudhibiti baadhi ya maeneo muhimu mashariki ya Ukraine
Wanajeshi wa Ukraine wameendelea kukabiliana na mamluki wa Urusi Wagner kudhibiti baadhi ya maeneo muhimu mashariki ya Ukraine AP - LIBKOS
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa mauzo na masoko Poven Kumaresan amesema vifaa hivyo ambavyo ni mfano wa silaha za kivita vimekuwa vikiuzwa kwa serikali nyingi duniani, na sio Ulaya pekee, huku akikiri kuwa pato liliongezeka kwa asilimia 100 katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Kumaresan anasema kuna mbinu nyingine ambayo wamebuni katika kutumia ufundi mwengine wa siri kama puto lililojazwa hewa ambalo hutumiwa badala ya silaha halisi katika kumpumbaza adui kwenye uwanja wa vita.

Hata hivyo Wasimamizi wa kampuni ya Inflatech wamekataa kuthibitisha kuuza bidhaa zao kwa Ukraine, wakitaja usiri wa kijeshi, lakini walikiri kuwa dazeni tatu ya wafanyikazi wake kwa sasa wanazalisha mizinga  kughushi, magari ya kivita na hata ndege za kivita kati ya 30 au 40 kwa mwezi, na kwamba soko la mauzo linazidi kuongezeka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.